Pata taarifa kuu
IRAQ-SIASA

Iraq: Chama cha kiongozi wa kishia chaelekea kutangazwa mshindi wa uchaguzi

Nchini Iraq, chama kiliopewa jina la kiongozi wa Kishia Muqtada al-Sadr kinaaelekea kupata ushindi kwenye Uchaguzi wa wabunge uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Wafuasi wa Moqtada al-Sadr wakiwa na furaha, baada ya chama chao kutangazwa kuelekea kupata ushindi wa uchaguzi wa wabung, Baghdad, Oktoba 11, 2021.
Wafuasi wa Moqtada al-Sadr wakiwa na furaha, baada ya chama chao kutangazwa kuelekea kupata ushindi wa uchaguzi wa wabung, Baghdad, Oktoba 11, 2021. AFP - AHMAD AL-RUBAYE
Matangazo ya kibiashara

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi yanaonesha kuwa, aliyekuwa Waziri Mkuu Nouri al-Maliki anatarajiwa kupata ushindi miongoni mwa vyama vya Kishia.

Matokeo ya awali katika mwelekeo huu yalitanazwa Jumatatu usiku, na huenda akapata viti vingi kwani matokeo ya uchaguzi bado yanaendelea kutangazwa.

Ushindi wa chama cha kiongozi wa Kishia Moqtada al-Sadr ulitarajiwa. Leo matokeo ni ya kushangaza, amebaini mwandishi wetu huko Baghdad, Lucie Wassermann.

Kwa sasa, kwa kuzingatia matokeo haya ya kwanza, Mhubiri huu wa Ushia mwenye ushawishi mkubwa anaonekana tena kutokuwa  na mshindani, wakati hapo katika mwaka wa 2018 alikaribiana kura na kambi zingine.

"Watu lazima washerehekee ushindi huu wa kambi kubwa zaidi (...) bila kusababisha uharifu", Bwana Sadr amesema kwenye hotuba iliyorushwa kwenye runinga nchini Iraq.

Wakati wa jioni, Uwanja wa Tahrir katikati mwa Baghdad, wafuasi wa chama hiki walikusanyika wakibebelea bendera za nchi ya iraq, bendera za chama chao pamoja na picha za kiongozi wao.

Kulingana na afisa wa wa chama cha Muqtada al-Sadr, aliyehojiwa na shirika la habari la AFP, chama hiki kinaweza kupata "takriban viti 73", kati ya jumla ya viti 329.

Afisa wa tume ya uchaguzi, ambaye aliomba jina lake lisitajwe, alikuwa amethibitisha kwa AFP kwamba sasa chama cha kiongozi wa Kishia Muqtada al-Sadr "kinaongoza", kulingana na matokeo ya awali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.