Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA-USALAMA

Joto la kisiasa laanza kupanda nchini Uganda kuelekea Uchuguzi Mkuu mwakani

Naibu Waziri wa Kazi nchini Uganda Mwesigwa Rukutana anazuiwa na polisi baada ya kumpiga risasi mfuasi wa mpinzani wake, wakati wa zoezi la kura ya mchujo kuwania ubunge kupitia chama tawala NRM kuelekea Uchaguzi Mkuu mapema mwaka 2021.

Mpja ya maeneo ya mji mkuu wa Uganda, Kampala.
Mpja ya maeneo ya mji mkuu wa Uganda, Kampala. REUTERS/James Akena/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Mwesigwa Rukutana amefunguliwa mashtaka ya mauaji na kuchochea machafuko ya kisiasa, wakati huu taifa hilo la Afrika Mashariki likianza kushuhudia joto la kisiasa.

Rais Yoweri Museveni amesema hakuna atakayevulimiwa kwa kuchochea machafuko ya kisiasa nchini Uganda.

Hivi karibuni mwanasiasa mkongwe wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye, ambaye amewahi kuwania urais mara nne, alitangaza kuwa hatawania tena wadhifa huo wakati wa Uchaguzi Mkuu ambao umepangwa kufanyika mapema mwaka 2021.

Besigye aliwaambia wafausi wa chama chake cha FDC kuwa baada ya kutafakari kwa kina, ameona kutia nafasi kwa mtu mwingine kushiriki kwenye Uchaguzi huo.

Mwaka 2019 Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Waine na Dkt Kizza Besigye waliahidi kushirikiana kukiondosha madarakani chama tawala, National Resistance Movement (NRM) kinachoongozwa na rais Yoweri Museveni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.