Pata taarifa kuu
UGANDA-EU-BOBI WINE-SIASA-USALAMA

Ujumbe wa Ulaya wakutana kwa mazungumzo na Bobi Wine

Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Uganda, umekutana na kufanya mazungumzo ya faragha na kiongozi wa chama cha NUP na vuguvugu la People Power Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Hivi karibuni Robert Kyagulanyi, mkosoaji mkubwa wa utawala wa Museveni, alizindua chama kipya kinachojulikana kama National Unity Platform kuelekea Uchaguzi Mkuu mapema mwaka 2021.
Hivi karibuni Robert Kyagulanyi, mkosoaji mkubwa wa utawala wa Museveni, alizindua chama kipya kinachojulikana kama National Unity Platform kuelekea Uchaguzi Mkuu mapema mwaka 2021. AFP Photos/ Guillem Sartorio
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu umekuja wakati huu Bobi Wine akisema, mchakato wa chama chake kushiriki kwenye Uchaguzi huo unatatizwa na serikali ya rais Yoweri Museveni.

Hivi karibuni Robert Kyagulanyi, mkosoaji mkubwa wa utawala wa Museveni, alizindua chama kipya kinachojulikana kama National Unity Platform kuelekea Uchaguzi Mkuu mapema mwaka 2021. Chama amabacho alisema kitakuwa chini ya vuguvugu aliloanzisha la People Power.

Nacho chama tawala nchini Uganda cha NRM kilimuidhinisha rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museveni kuongoza taifa hilo kwa muhula wa sita mfululizo.

Museveni anatarajiwa kukabiliana na mbunge wa upinzani Robert Kyagulanyi, anayefahamika kwa jina la Bobi Wine, ambaye anatarajiwa kuwania kiti cha urais.

Mwaka 2017 bunge la Uganda lenye wabunge wengi wa chama cha NRM, liliondoa ukomo wa umri wa rais, jambo lililokuwa kikwazo kwa rais Museveni kuwania tena kiti cha urais, na hivyo kumuwezesha kuwania urais.

Iwapo Rais Museveni atachaguliwa kuiongoza Uganda kwa muhula mwingine wa sita wa miaka mitano, atakuwa ameliongoza taifa la Afrika Mashariki kwa miaka arobaini, na anaweza kuongoza miaka zaidi iwapo atataka kufanya hivyo.

Rais Museveni ameliongoza taifa la Uganda kwa miaka 34, akiwa ni rais wa tatu barani afrika kuwa madarakani kwa miaka mingi zaidi, baada ya Rais wa Guinea Equatorial Teodoro Obiang ambaye amehudumu kwa miaka 41 akifuatiwa na rais wa Cameroun Paul Biya, ambaye amehudumu kwa miaka 38.

Wakati hayo yakijiri, ripoti nchini humo zinasma mwanasiasa mkongwe wa upinzani Kizza Besigye huenda asigombee urais mwaka ujao, hali ambayo huenda ikaleta ushindani mpya wa kisiasa nchini humo.

Ingawa tarehe rasmi ya Uchaguzi Mkuu wa Uganda haijatangazwa, inatarajiwa kuwa uchaguzi huo utafanyika Februari 2021, kulingana na vyanzo vilivyo karibu na utawala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.