Pata taarifa kuu
KENYA-MAANDAMANO-UCHAGUZI

Joto la kisiasa lapamba moto siku tatu kabla ya uchaguzi Kenya

Siku tatu kabla ya uchaguzi wa urais nchini Kenya ambao umepangwa kufanyika Alhamisi Oktoba 26, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC, Wafula Chebukati, amemualika Jumatatu hii rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mazungumzo kuhusu uchaguzi na mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

Maandamano ya upinzani jijini Nairobi nchini Kenya
Maandamano ya upinzani jijini Nairobi nchini Kenya Photographer James Shimanyala's - copyright RFI"
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita Wafula Chebukati alikutana na kiongozi wa muungano wa upinzani Raila Odinga.

Mapema wiki iliyopita Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC aliomba mazungumzo ya moja kwa moja kati ya rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga. Mazungumzo ambayo yalifutiliwa mbali na rais Kenyatta.

Raila Odinga alitangaza kutoshiriki uchaguzi wa Oktoba 26. Lakini baada ya kukutana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, alilegeza msimamo na kusema anaweza kubadilisha mawazo na kurejea kwenye kinyang'anyiro cha kuwania urais iwapo kutakuwa na mazungumzo na kufanyika kwa mageuzi ndani ya Tume ye Uchaguzi.

Awali alitolea wito wafuasi wake kufanya maandamano makubwa siku ya uchaguzi.

Makabiliano kati ya wafuasi wa upinzani na vikosi vya usalama yamekua yakishuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini Kenya. Makabiliano hayo yamesababisha vifo vya watu kadhaa na wengine wengi kukamatwa.

Mashirika mbalimbali ya haki za binadamu yamekua yakitoa wito wa utulivu na kuvumialiana. Uchaguzi mpya wa urais umepangwa kufanyika Oktoba 26, baada ya Mahakama ya Juu nchini humo kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti 8, ambapo Rais Uhuru Kenyatta aiibuka mshindi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.