Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI-HAKI

Chama cha Kenyatta chaomba Raila Odinga afunguliwe mashitaka

Chama cha Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta kimekwenda katika Mahakama ya Juu kumshtaki kiongozi wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga kwa kutangaza maandamano ya nchi nzima ili kuzuia Uchaguzi mpya wa urais wiki ijayo.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwa na naibu wake William Ruto baada ya kutangaza kuundwa kwa chama kipya cha Jubilee
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwa na naibu wake William Ruto baada ya kutangaza kuundwa kwa chama kipya cha Jubilee Kenya State House
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa chama hicho Raphael Tuju amesema, kauli ya Odinga inakwenda kinyume na agizo la Mahakama hiyo iliyotaka Uchaguzi mpya kufanyika ndani ya siku 60.

Hayo yanajiri wakati Raila Odinga alikutana Alahamisi hii na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC, Wafula Chebukati, na kusema kuwa anaweza kubadilisha mawazo na kurejea kwenye kinyanganyiro cha kuwania urais iwapo kutakuwa na mazungumzo na kufanyika kwa mageuzi ndani ya Tume ye Uchaguzi.

Mkutano huu umekuja baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati siku ya Jumatano kuomba mazungumzo ya moja kwa moja kati ya rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema, anaweza kubadilisha mawazo na kurejea kwenye kinyanganyiro cha kuwania urais iwapo kutakuwa na mazungumzo na kufanyika kwa mageuzi ndani ya Tume ye Uchaguzi.

Uhuru Kenyatta kwa upande wake, akiendelea na kampeni za kisiasa amesema kuwa mazungumzo pekee anayoweza kushiriki ni kuhusu namna Uchaguzi wa wiki ijayo utakavyofanyika kwa amani.

Hii ni dalili kuwa huenda mwafaka usipatikane hivi karibu kuhusu Uchaguzi wa tarehe 26.

Odinga ameitisha maandamano ya nchi nzima siku ya kupiga kura, hali ambayo imeendelea kuzua wasiwasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.