Pata taarifa kuu
KENYA-IEBC-UCHAGUZI

Afisa mkuu mtendaji wa tume ya Uchaguzi kutoshiriki uchaguzi wa Oktoba 26

Kamishna mkuu wa tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC huenda asishiriki uchaguzi wa Oktoba 26 na tayari anaaza likizo yake ya wiki tatu. Uchaguzi mpya utarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi Oktoba 26, Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation nchini Kenya.

Maandamano ya NASA, muungano wa upinzani nchini Kenya, yakitawanywa na polisi ikitumia gesi ya machozi, Nairobi, Oktoba 16, 2017.
Maandamano ya NASA, muungano wa upinzani nchini Kenya, yakitawanywa na polisi ikitumia gesi ya machozi, Nairobi, Oktoba 16, 2017. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Ezra Chiloba ni Afisa mkuu mtendaji wa Tume ya Uchaguzi IEBC. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation Bw Chiloba amekuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka muungano wa upinzani Nasa kujiuzulu.

Chiloba anachukua likizo baada ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wafula Chebukati kutaka maafisa waliotajwa baada ya uchaguzi huo kufutiliwa mbali kung'atuka, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation Chiloba anaamini kwamba kutoshiriki kwake uchaguzi wa Oktoba 26 hakutaathiri maandalizi ya Tume ya Uchaguzi kusimamia uchaguzi ulio huru na haki .

Kuna mashaka ya kutofanyika uchaguzi Oktoba 26 nchini Kenya. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, IEBC, amesema kuwa kwa mazingira ya sasa itakua vigumu kuandaa uchaguzi wa kuaminika Alhamisi ijayo Oktoba 26.

Kiongozi wa muungano wa upinzani Raïla Odinga amekata kushiriki uchaguzi huo na kuwataka wafuasi wake kuandamana siku hiyo ya kura.

IEBC ilikua ikijaribu kuandaa mkutano na wagombea wote lakini mpango ulifeli. Mvutano unaendelea kuongezeka na mashirika mbalimbali yanaomba jumuiya ya kimataifa kuingilia kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.