Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Polisi nchini Kenya yasema waandamanaji wanne waliuawa wakati wa maandamano

Wizara ya Mambo ya ndani nchini Kenya inasema watu wanne walipoteza maisha na polisi 10 kujeruhiwa katika maandamano ya wafuasi wa upinzani, kushinikiza mabadiliko ndani ya Tume ya Uchaguzi.

Polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwasambaratisha waandamanaji wa upinzani jijini Nairobi
Polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwasambaratisha waandamanaji wa upinzani jijini Nairobi REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yalifanyika katika maeneo mbalimbali nchini humo kati ya tarehe 2 na 16 mwezi Oktoba, waandamanaji wengine saba walikamatwa.

Msemaji wa Jeshi la Polisi George Kinoti amesema kuwa mali yenye thamani ya Shilingi za Kenya Milioni 6, iliharibika baada ya kuvamiwa kwa duka la Jumla la Tumaini mjini Kisumu.

Aidha, amesema kuwa jeshi la Polisi linachunguza namna waandamanaji hao walivyopoteza maisha lakini pia kuchunguza namna uharibifu wa mali ulivyofanyika.

Wanasiasa wa upinzani wamelishutumu jeshi la Polisi kwa kuwauwa wafuasi wake, madai ambayo polisi wamekanusha.

Maeneo yaliyoathiriwa ni jijini Nairobi, Mombasa, Kisumu na maeneo mengine nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.