Pata taarifa kuu
KENYA-MAANDAMANO-UCHAGUZI

Polisi ya Kenya yashtumiwa kuwaua kwa makusudi waandamanaji

Mashirika mawili ya Haki za Binadamu yameiomba serikali ya Kenya kuchunguza na kuwachukulia hatua za kisheria maafisa wa polisi wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya watu wengi wakati wa maandamano yaliyoitishwa na upinzani wiki iliyopita kutaka kufanyike mageuzi katika Tume ya Uchaguzi IEBC.

Polisi ya Kenya ikisambaratisha maandamano ya muungano wa upinzani wa National Super Alliance (NASA) katika mitaa ya Nairobi
Polisi ya Kenya ikisambaratisha maandamano ya muungano wa upinzani wa National Super Alliance (NASA) katika mitaa ya Nairobi REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilitokea baada ya siku moja ya serikali kupiga marufuku maandamano katikati mwa miji mikubwa mitatu nchini humo.

Serikali ya Kenya imepiga marufuku maandamano katika maeneo ya katikati mwa miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu.

Jumatano wiki iliyopita Kaimu waziri wa usalama Dkt Fred Matiang'i alisema kwamba wanaopanga maandamano wanafaa kuwajibishwa kutokana na uharibifu wa mali unaotokea wakati wa maandamano.

Hatua ya Dkt Matiang'i ilitokea huku muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) unaoongozwa na Raila Odinga ukiendelea na maandamano ya kushinikiza mageuzi katika Tume ya Uchaguzi (IEBC).

Siku ya Jumanne Oktoba 10 kiongozi wa muungano wa upinzani Raila Odinga alitangaza kujiuzulu katika uchaguzi wa Oktoba 26.

Hivi karibuni ripoti ya shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International na Human Right Watch iliwahusisha polisi na mauaji ya karibu watu karibu 70 nchi nzima. Nusu ya mauaji hayo yakitokea katika mji wa Nairobi.

Ripoti hiyo pia imewalaumu polisi kwa kuongeza hali ya wasiwasi kutokana na operesheni zake katika maeneo yanayoonekana kuwa ngome ya upinzani.

Watu wengi wameuawa tangu kuzuka kwa maandamano ya upinzai nchini humo, huku wengine wengi wakikamatwa na polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.