Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI-MAHAKAMA

Mawakili wa upinzani wadai kuwa Tume ya Uchaguzi imeshindwa kutekeleza amri ya Mahakama

Mawakili wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, wanasema wamenyimwa nafasi ya kuangalia mitambo ya Tume ye Uchaguzi IEBC, kama ilivyoagizwa na Mahakama ya Juu siku ya Jumatatu.

Majaji wa Mahakama ya Juu nchini Kenya
Majaji wa Mahakama ya Juu nchini Kenya www.reuters.com
Matangazo ya kibiashara

Wakili wa kiongozi wa upinzani Paul Mwangi, amesema kuwa hawajaruhusiwa kuangalia mitambo hiyo na hivyo wanarejea Mahakamani kuwaambia Majaji walichokipata.

“Nipo katika Tume ya Uchaguzi, tumechezewa mchezo hapa, hatujaruhusiwa kuangaliwa mitambo hiyo na kuisoma, tunarejea Mahakamani,” amesema Paul Mwangi.

Hata hivyo, Mawakili wa Tume ya Uchaguzi hata hivyo wanasema kuwa wametimiza agizo hilo, baada ya Mahakama kuamuru hapo jana kuwa, upinzani wana haki ya kusoma na kuangalia mitambo hiyo inayoaminiwa kutunza matokeo yanayoaminiwa kuwa sahihi.

Wakili Paul Muite, aliihakikishia Mahakama kuwa Tume ya Uchaguzi ingetekeleza hatua hiyo.

Mahakama inarejelea vikao vyake saa tano asubuhi.

Siku ya Jumatatu, Mawakili wa upinzani waliwasilisha kesi yao kupinga ushindi wa Kenyatta huku wakiwaambia Majaji kuwa, kulikuwa na wizi mkubwa na Kenyatta hakushinda kwa haki.

Mawakili wa Kenyatta na Tume ya Uchaguzi wanawasilisha utetezi wao hivi leo.

Uamuzi wa mwisho utatolewa siku ya Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.