Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Kesi kupinga ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kuanza kusikilizwa leo

Hatua ya pili katika Kesi ya kupinga ushindi wa rais wa Kenya Uhuru Kenyata inatarajiwa kuanza leo jioni baada ya kumalizika kwa hatua ya kwanza hapo jana kwa pande zote tatu yaani upande wa NASA, Jubilee na IEBC kuwasilisha mahakamani hoja zao za maandishi.

Rais mteule Uhuru Kenyatta na hasimu wake Raila Odinga
Rais mteule Uhuru Kenyatta na hasimu wake Raila Odinga Photo: AFP/Jennifer Huxta
Matangazo ya kibiashara

Kikao cha kwanza kitawakutanisha majaji saba wa mahakama kuu , na mawakili wa pande zote tatu kukubaliana utaratibu wa namna kesi hiyo itakavyokwenda.

Maswali ya msingi yatakayoibuliwa katika kesi hii ni pamoja na kama makosa yaliyotajwa katika fomu za data yatakuwa na uwezo wa kubadilisha matokeo ya kura, na ikiwa rais Uhuru Kenyatta alitumia mamlaka yake vibaya katika kuchunguza masanduku zaidi ya elfu 40 pamoja na kuingilia mfumo wa tume hiyo.

Kesi hiyo itaanza saa moja usiku leo Jumamosi kutokana na jaji mkuu David Maraga ambaye ni msabato atakuwa akitekeleza ibada ya Sabato.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.