Pata taarifa kuu
KENYA-KISUMU-UCHAGUZI

Wakazi wa Kisumu: Odinga kaibuka mshindi wa uchaguzi wa urais Kenya

Wakazi wa eneo la Kisumu wamesubiri kwa hamu na gamu ili Tume ya Uchaguzi (IEBC) iweze kumtangaza mshindi, huku wengi wao wakiwa na imani kuwa Raila Odinga ambaye amebobea eneo hilo ataibuka mshindi.

Mbele ya kituo cha kupigia kura karibu na Baragoy, katika akaunti ya Samburu (kaskazini mwa Kenya), Jumanne August 8.
Mbele ya kituo cha kupigia kura karibu na Baragoy, katika akaunti ya Samburu (kaskazini mwa Kenya), Jumanne August 8. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kinara wa upinzani, Raila Amolo Odinga kuhutubia taifa na kuelezea kutoridhishwa na matokeo yanayotolewa na tume ya IEBC hisia mbali mbali zimekua zikitolewana wakazi wa eneo la Kisumu, huku wengi wao wakiitaka tume hiyo  kuhakikisha kuwa inatenda haki.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walizungumza na mwandishi wetu Marion Mwange, kuhusiana na iwapo wana imani na Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC).

Hata hivyo hapo awali kuliwezwa kushuhudiwa maandamano kutoka eneo la Kondele viungani mwa mji wa kisumu huku wakazi wakielezea kusikitishwa kwao na jinsi Tume ya Uchaguzi inaendeleza na zoezi la kuhesabu kura hasa kwa nafasi ya urais.

Polisi hata hivyo waliweza kuingilia kati na kutuliza hali hiyo.

Naye James Shimanyula mwandishi wetu katika ukanda wa Afrika Mashariki, alimhoji Bernard Muleng’ani, kutoka Uganda aliyewakilisha bunge la Afrika Mashariki kama mchunguzi katika uchaguzi wa Kenya, amepongeza maandalizi ya uchaguzi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.