Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Odinga ayakataa matokeo, asema kura zake zimebadilishwa

Mgombea wa upinzani katika Uchaguzi wa urais nchini Kenya Raila Odinga, ametangaza rasmi kutoyatambua matokeo ya urais yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Uchaguzi IEBC.

Raïla Odinga
Raïla Odinga Reuters / Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Odinga akizungumza na wanahabari jijini Nairobi, amesema wamebaini kuwa mtandao unaojumuisha matokeo hayo umedukuliwa na kumpa ushindi rais Kenyatta.

Matokeo hayo yameendelea kujumuisha katika ukumbi wa Bomas of Kenya.

“Tunawaomba Wakenya wayakatae matokeo haya,” alisema Raila.

“Hakuna Uchaguzi uliofanyika,” ameongeza Odinga.

Aidha, ameongeza kuwa, matokeo yake yalipunguzwa karibu katika Kaunti zote 47 nchini humo lakini pia yakaathiri matokeo ya wagombea wa Magavana, Maseneta na hata wabunge.

Odinga ameeleza kuwa Uchaguzi huu ulikuwa ni wa kihistoria lakini kwa bahati mbaya, umeharibiwa kwa kuingiliwa na serikali ya Jubilee.

“Watu wa Jubilee ndio walioingilia na kudukua mtandao wa IEBC,” aliongeza.

Hata hivyo, Odinga amewataka Wakenya kutulia wakati huu wakiendelea kuchunguza kwa kina kuhusu kuingiliwa kwa matokeo haya.

Alipoulizwa kuhusu kituo cha upinzani cha kujumuisha matokeo, Odinga amesema kuwa hesabu zao zinaonesha kuwa alishinda Uchaguzi huo kwa kupata kura Milioni 8.2 huku Kenyatta akipata kura Milioni 7.2.

Haya yote yamekuja wiki moja tu baada ya Meneja wa Teknolojia katika Tume ya Uchaguzi IEBC kuuawa katika mazingira ya kutatanisha Chris Msando.

Wakati uo huo, Tume ya Uchaguzi imeendelea kutangaza matokeo na kuonesha kuwa rais Kenyatta anaendelea kuongoza kwa zaidi ya 54 huku Odinga akiwa na asilimia 44.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.