Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya: Matokeo mnayoyaona sio ya mwisho

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya inasema matokeo yanayooneshwa katika vyombo vya Habari nchini humo sio rasmi wala sio ya mwisho.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBCKenya
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati amesema kinachoendelea kwa sasa ni kusubiri  fomu rasmi za 34 A na 34 B ili kulinganisha na kujumuisha matokeo rasmi.

Fomu 34 A, inaonesha matokeo yaliyotangazwa katika vituo vya kupigia kura huku ile ya 34 B, ikionesha matokeo yalitangazwa katika maeneo bunge.

Aidha, Chebukati amewaomba Wakenya kuwa watulivu kipindi hiki wanapopitia matokeo yote ambayo hayawezi kubadilishwa baada ya kutangazwa katika maeneo bunge.

Pamoja na hilo, amesema kuwa wanashirikiana na wadau wote kuhakikisha kuwa kila kitu kinakuwa sawa kabla ya kutangaza matokeo ya mwisho kwa sababu, sheria inawapa siku saba kutangaza matokeo ya urais.

Kuhusu madai ya muungano wa upinzani NASA, kuwa mfumo wa IEBC umeingiliwa na matokeo kubadilishwa, Chebukati amesema wanauamini mfumo wao lakini wanachunguza madai hayo.

Raila Odinga anayewania urais kupitia muungano wa NASA, amekataa kuyatambua matokeo hayo na kudai wizi wa kura umefanyika.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.