Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Shughuli za kawaida zarejea polepole nchini Kenya

Shughuli za kawaida hazijarejea katika maeneo mengi nchini Kenya, siku moja baada ya wapiga kura kujitokeza kupiga kura siku ya Jumanne.

Mtaa wa Moktar Daddah jijini Nairobi
Mtaa wa Moktar Daddah jijini Nairobi wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Utulivu unashuhudiwa lakini kuna hali ya wasiwasi, kutokana na namna matokeo ya urais yanavyoendelea kutangazwa.

Mwandishi wa RFI Magharibi mwa nchi hiyo Marion Mwange, anaripoti kuwa, watu wana wasiwasi lakini utulivu unashuhudiwa.

“Hapa Kisumu, watu wanaonekana kukataa tamaa kwa sababu ya matokeo wanayoyasikia,” amesema Marion.

Kumekuwa na ripoti kuwa Polisi wamekabiliana na waandamanaji katika mtaa wa Kondele mjini Kisumu, waliojitokeza kupinga matokeo ya urais.

Jijini Nairobi, watu wengi hawajakwenda kazini huku maduka mengi yakiendelea kufungwa kwa hofu lakini watu wameonekana wakitembea jijini.

“Hapa Nairobi, naona shughuli zinaendelea polepole lakini maduka bado yamefungwa, kuna utulivu lakini wasiwasi,” ametuambia Mwandishi wetu Emmanuel Makundi.

Mjini Mombsa, maafisa wa usalama wamekanusha madai ya kuwepo kwa maandamano kupinga matokeo ya urais na kuyaita ni propaganda.

Mwandishi wa RFI mjini Mombasa, Joseph Jira amesema shughuli zimeanza kkurejea pole.

“Mambo hayajarejea kama kawaida lakini magari yapo na watu wapo mjini,” amesema Jira.

Waziri wa Usalama Fred Matiang'i amesema kuwa hali ni shwari nchi nzima na kuwataka Wakenya kurejea kazini.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.