Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

IEBC yasema haina mpango wa kusitisha zabuni ya kuchapisha karatasi za kupigia kura

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya inasema haitaondoa zabuni iliyotoa kwa kampuni ya Dubai kuchapisha karatasi za kupigia kura kuelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Wafula Chebukati
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Wafula Chebukati IEBC
Matangazo ya kibiashara

IEBC inasema ililipa kampuni hiyo Dola za Marekani 24.2 kuchapisha mamilioni za karatasi hizo na haina nia ya kuipokonya kiazi hiyo.

Mgombea wa muungano wa upinzani Raila Odinga amedai kuwa viongozi wa kampuni hiyo inayofahamika kama Al-Ghurair wana ushirikiano wa karibu na rais Uhuru Kenyattaa na Familia yake, na hivyo haiaminiki.

Mapema wiki hii, Odinga alisema Kenyatta ambaye anawania urais kwa muhula wa pili, alikutana na kiongozi wa kampuni hiyo mara kadhaa ndani na nje ya nchi, hatua ambao amesisitiza inaathiri uwazi wa Uchaguzi huo.

Upinzani unataka Tume ya Uchaguzi kuachana na kampuni hiyo na kutafuta nyingine kwa madai kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa kuchapishwa kwa karatasi zaidi ili kumsaidia rais Kenyatta kuibuka mshindi.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati, amekanusha madai ya upinzani na kusema kampuni hiyo ilikidhi vigezo vyote kabla ya kupewa kazi hiyo.

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wamelaani upinzani kwa kutoa madai hayo na kusema ni dalili kuwa Odinga anataka uchaguzi usifanyike mwezi Agosti.

Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema, Tume ya Uchaguzi ina kazi kubwa kuhakikisha kuwa Wakenya wana imani na kazi yao na uchaguzi wa mwezi Agosti utakuwa huru na haki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.