Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Wanasiasa nchini Kenya wakubaliana kuhusu muundo wa IEBC

Kamati maalum ya wanasiasa wa serikali na upinzani nchini Kenya, imekubaliana kuhusu muundo na mfumo wa Tume mpya ya Uchaguzi IEBC.

Maandamano ya upinzani miezi kadhaa zilizopita kutaka mabadiliko katika Tume ya Uchaguzi
Maandamano ya upinzani miezi kadhaa zilizopita kutaka mabadiliko katika Tume ya Uchaguzi REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Imekubaliwa kuwa Tume hiyo itakayoundwa hivi karibuni, itakuwa na Makamishena saba.

Suala hili lilitishia kusambaratisha mazungumzo haya ya wanasiasa wa CORD na Jubilee ambao wamekuwa wakikutana kwa wiki tatu sasa kujadili mabadiliko kuhusu Tume ya Uchaguzi.

Upinzani ulitaka Tume hiyo mpya iwe na Makamishena saba, huku upande wa serikali ukitaka Makamishena tisa.

Aidha, imekubaliwa kuwa Makamishena hao wapya watakaoteuliwa na Kamati maalum watakuwa wa kudumu, kinyume na muda mfupi kama upinzani ulivyokuwa unapendekeza.

Baada ya makubaliano hayo, imeamuliwa kuwa Makamishena wa sasa wataondoka Ofisini kufikia tarehe 30 mwezi Septemba baada ya kupatikana kwa Makamishena wapya.

Kamati hiyo imemaliza mazungumzo yake siku ya Jumanne, na sasa inaanda ripoti itakayowasilishwa bungeni ili kujadiliwa na kupitishwa na wabunge.

Mazungumzo haya yalikuja baada ya upinzani kuongoza maandamano ya kitaifa kushinikiza kujiuzulu kwa Makamishena wa sasa kwa madai kuwani wafisadi na wanaipendelea serikali.

Kenya inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2017.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.