Pata taarifa kuu
EU-BURUNDI

EU yalaani shambulizi dhidi ya Willy Nyamitwe mjini Bujumbura

Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Burundi umelaani shambulizi dhidi ya Willy Nyamitwe, Mshauri mkuu wa wa rais wa Burundi katika masuala ya mawasiliano.

Willy Nyamitwe alishambuliwa kwa risasi Jumatatu usiku wiki hii na watu ambao hawajajulikana, huku mmoja wa walinzi wake na dereva wakiuawa.
Willy Nyamitwe alishambuliwa kwa risasi Jumatatu usiku wiki hii na watu ambao hawajajulikana, huku mmoja wa walinzi wake na dereva wakiuawa. © Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, Umoja wa Ulaya (EU) umelaani shambulizi hilo ambalo umelitaja kuwa ni kitendo kisichokubalika.

Kitendo hiki "kinaonyesha hali ya wasiwasi na vurugu vinavyojiri nchini Burundi, kutokana na mauaji mbalimbali na visa vya watu kutoweka bila kiholela," Umoja wa Ulaya umebaini.

Umoja wa Ulaya umeongeza kuwa "ghasia za kisiasa, zozote zile hazikubaliki".

Umoja wa Ulaya umesema unaunga mkono jitihada za rais wa zamani wa Tanzania Banjamin Mkapa kwa kuwasuluhisha Warundi. Umoja wa Ulaya umekumbusha kwamba "ufumbuzi wa kisiasa kwa njia ya mazungumzo yatakayowasirikisha wadau wote ndio njia sahihi ya kupelekea nchi hiyo inaondokana na mgogoro huo, na hali hiyo ndio itakayo rejesha amanina usalama nchini Burundi ".

Willy Nyamitwe alishambuliwa kwa risasi Jumatatu usiku wiki hii na watu ambao hawajajulikana, huku mmoja wa walinzi wake na dereva wakiuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.