Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-USALAMA

Willy Nyamitwe aponea kuuawa mjini Bujumbura

Mshauri mkuu wa rais wa Burundi anayehusika na maswala ya mawasiliano, Willy Nyamitwe ameponea kuuawa baada ya kundi la watu kushambulia gari lake alipokua akikaribia nyumbani kwake eneo la Kajaga Kilomita 7 kutoka mjini Bujumbura.

Willy Nyamitwe, conseiller du président burundais Pierre Nkurunziza.
Willy Nyamitwe, conseiller du président burundais Pierre Nkurunziza. DR
Matangazo ya kibiashara

Willy Nyamitwe, Mshauri wa Rais Pierre Nkurunziza anayehusika na mawasiliano, ameponea kuuawa alipokua akikaribia kuwasili nyumbani kwake usiku wa Jumatatu Novemba 28, eneo la Kajag, mtaani Rukaramu mkoani Bujumbura vijijini, kilomita 7 na mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura. Askari mmoja mongoni mwa walinzi wake aliuawa na mwengine kujeruhiwa. Watu hao walioendesha shambulio hilo hawajajulikana.

Habari ambayo haijathibitishwa na serikali na imeendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Burundi. Lakini inaarifiwa kuwa Willy Nyamitwe anapewa matibabi katika hospitali ya Kira Hospital mjini Bujumbura, baada ya kujeruhiwa kwa risasi mkononi.

"Nakusifu Mungu kwa kumuepusha na kifo ndugu yangu Willy Nyamitwe usiku ambaye aliponea jaribio jingine lililolenga kumumalizia maishai. Utukufu ni wake Mungu, " kakake Alain Nyamitwe, ameandika kwenye Twitter.

Willy Nyamitwe ambaye ni mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa katika chama tawala cha CNDD-FDD na utawala wa Pierre Nkurunziza amekua akilaumiwa na upinzani na mashirika ya kiraia yaliyo uhamishoni nje ya kuwa amekua akitoa maneno mabaya dhidi yao.

Hata hivyo Afisa huyo amekua akilaumi na baadhi ya wa fuasi wa chama tawala kwa kuendelea kuchochoea chuki inayolenga kukigawa chama hiki.

Chama cha CNDD-FDD kinaendelea kukabiliwa na malumbano ya ndani, ambapo baadhi ya wafuasi wanabaini kwamba chama hiki kinaongozwa na maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi na polisi waliotoka katika chama hicho wakati kilipokua kikiendesha viuta vya maguguni wamesem akuwa wafuasi hawana kauli katika chama hicho.

Hali ya usalama imeendelea kudorora nchini Burundi, na machafuko yaliyoikumba nchi hiyo tangu rais Pierre Nkurunziza kuchuku uamuzi wa kuwania muhula mwengine, yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 600 kwa mujibu wa mashirika ya kiraia, na watu zaidi ya 250,000 kuyakimbia makazi yao na kukimbilia katika nchi jirani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.