Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-USALAMA

Mwanasiasa wa upinzani akamatwa kusini mwa Burundi

Nchini Burundi duru za usalam zinaarifu kwamba mwanasiasa wa upinzani nchini humo Gervais Niyongabo alikamatwa Jumatano kwa kosa la "kuhatarisha usalama wa taifa". Bw Niyongabo alikamatwa mkoani Makamba, kusini mwa Burundi.

Bujumbura, Februari 3, 2016. Burundi, mzunguko wa vurugu na ukandamizaji vinandelea kushuhudiwa kwa mwaka mmoja sasa.
Bujumbura, Februari 3, 2016. Burundi, mzunguko wa vurugu na ukandamizaji vinandelea kushuhudiwa kwa mwaka mmoja sasa. © REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimana
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi ya Burundi, Pierre Nkurikiye, mwanasiasa huyo kwa sasa anazuiliwa mjini Bujumbura na Idara ya Ujasusi (SNR), ambayo ni iko moja kwa moja chini ya mamlaka ya Rais Pierre Nkurunziza.

Idara ya Ujasusi ya Burundi inatuhumiwa na mashirika kadhaa ya kutetea haki za binadamu kutujihusisha na mateso dhidi ya wapinzani.

Wafuasi wengi kutoka upinzani nchini Burundi wameitoroka nchi hiyo kufuatia machafuko yaliyoikuba tangu mwezi Aprili 2015.

Machafuko hayo yalizuka kufuatia uamuzi wa Pierre Nkurunziza wa kuwania muhula mwingine katika uchaguzi wa irais uliyofanyika mwezi Julai 2015, baada kuchaguliwa kwa mara nyingine tena kwa muhula wa tatu, muhula ambao upinzani unautaja kuwa ni kinyume na katibaya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.