Pata taarifa kuu
BURUNDI-UN

UN: uhalifu dhidi ya ubinadamu nchini Burundi

Wachunguzi huru wa Umoja wa Mataifa wametoa orodha ya watuhumiwa ambao wanapaswa kufunguliwa mashitaka kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu ambao inawezekana kuwa ulitekelezwa nchini Burundi.

Askari polisi wakipiga doria katika mtaa wa mji wa Bujumbura, Aprili 12, 2016.
Askari polisi wakipiga doria katika mtaa wa mji wa Bujumbura, Aprili 12, 2016. STRINGER / cds / AFP
Matangazo ya kibiashara

Machafuko yaliyotokea nchini Burundi tangu Aprili 2015 kufuatia nia ya rais, Pierre Nkurunziza, ya kuwania muhula wa tatu katika ukiukaji mzima wa Mkataba wa amani na maridhiano wa Arusha. Hali ambayo ilisababisha maandamano na kupelekea kutokea kwa makabiliano makali kati ya raia na vikosi vya polisi, huku kukishuhudiwa mauaji ya watu kutoka hasa upande wa upinzani na wanaharakati wa haki za binadamu.

Uchaguzi wa Pierre Nkurunziza kwa mara nyingine mwezi Julai 2015 haukubadili chochote. Watu wanaendelea kuuawa na wengine kupotezwa, Idara ya Ujasusi, vikosi vya ulinzi na polisi vinanyooshewa kidole na upande mwengine makundi ya watu wenye silaha.

Visa vya kukamatwa kiholela na mateso

Wachunguzi huru wa Umoja wa Mataifa wamehitimisha kuwa ni vigumu kujua kiwango kamili cha uhalifu uliofanywa, "lakini tuna orodha ya maafisa waliohusika na visa hivi, " Christof Heyns aliyeshiriki katika uchunguzi huo amesema, akinukuliwa na Deutsche Welle. Wachunguzi wanasema kuwa wamekusanya ushahidi wa ubakaji, mauaji, kutoweka kwa watu, kukamatwa na kuteswa. Umoja wa Mataifa umeorodhesha watu 564 waliouawa nchini Burundi tangu mwezi Aprili 2015. Afisa mwandamizi wa zamani wa jeshi amewambia wachunguzi kwamba kuna orodha ya watu wanaotafutwa ili wauawe.

Ushahidi tosha

Mashahidi wamewataja maafisa 12 wa ngazi ya juu katika vikosi vya usalama ambao wamekua wakitoa taarifa moja kwa moja kwa serikali kama wanahusika na visa vya kutoweka kwa watu katika mazingira tatanishi.

Watu wanaodai kuwa waliteswa, wamesema kuwa walikua wakizuiliwa sehemu za siri, ikiwa ni pamoja na makazi ya rais na waziri mmoja ambaye hawakupendelea kumtaja. Aidha, kwa mujibu wa ripoti ya wachunguzi, miili ya watu waliouawa au kunyongwa imekua ikisafirishwa hadi kwenye mto Ruzizi, magharibi mwa Burundi na kuzikwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.