Pata taarifa kuu
BUUNDI-UFARANSA-UN

Burundi yapinga kutumwa kwa polisi wa Umoja wa Mataifa

Serikali ya Burundi imetoa rasmi msimamo wake Jumanne hii usiku baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha wiki iliyopita azimio linaloruhusu kupelekwa kwa askari polisi 228 wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi.

Balozi wa Burundi kwenye Umoja wa Mataifa, Albert Shingiro.
Balozi wa Burundi kwenye Umoja wa Mataifa, Albert Shingiro. UN Photo/Evan Schneider
Matangazo ya kibiashara

Askari polisi hawa watakua na kazi ya kujaribu kurejesha utulivu na kuheshimu haki za binadamu nchini humo. Lakini, serikali ya Burundi imeendelea na msimamo wako wa kupinga kikosi chochote kuingia katika ardhi yake.

Serikali ya Burundi, inasema imeshangazwakuona azimio hilo lilipitishwa kwa "haraka" na bila ridhaa yake. Kwa maani hiyo utawala wa Nkurunziza umekataa katu katu kupokea katika mazingira hayo kikosi hiki cha askari polisi wa Umoja wa Mataifa.

Katika nakala yenye pointi 18 iliyotolewa Jumanne usiku, Serikali ya Burundi imepinga uamuzi huo. Kutokana na kwamba azimio hili lilipitishwa bila ridhaa yetu, sheria ya Umoja wa Mataifa haikuheshimishwa. Upande wa usalama, majeshi yake yanadhibiti "kikamilifu hali ya mambo." "Kupelekwa kwa kikosi cha kigeni, Nakala hiyo inabaini, kunalenga tu kuandaa ngome kuu ya magaidi ambayo yamesambaratishwa."

Ufaransa na Rwanda, mahasimu wa sasa

Burundi inachukulia hali hii kwa kuzituhumu nchi hizi mbili ambazo inaona kama mahasimu wa sasa. Kwanza, nchini Rwanda, yanapewa mafunzo ya kijeshi "makundi ya kigaidi." Kisha Ufaransa, chanzo cha azimio la Umoja wa Mataifa, inajaribu kukosoa makosa iliyoyafanya nchini Rwanda mwaka 1994. "Jambo hilo halikubaliki kwamba Burundi ikubali kulipa gharama za maridhiano kati ya nchi hizo mbili kwa njia ya sadaka ya watu wake", serikali ya Burundi imesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.