Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA-MAUAJI

Mameya 2 wa zamani wa Rwanda wakana tuhuma dhidi yao

Kesi ya kihistoria imefunguliwa Jumanne hii Mei 10 nchini Ufaransa. Mameya wawili wa zamani wa wilaya ya Kabarondo wanatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Mahakama ya mji wa Paris.
Mahakama ya mji wa Paris. © Wikimedia Commons / Nitot
Matangazo ya kibiashara

Huu ni mwanzo wa wiki nane ambapo kesi hii itasikilizwa, na watuhumiwa hawa wawili wanakabiliwa na hukumu ya kifungo cha maisha jela kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya kimbari. Hata hivyo Octavien Ngenzi na Tito Barahira wamefutilia mbali thuma dhidi yao.

Octavien Ngenzi na Tito Barahira, ambao wanakanusha tuhuma hizo dhidi yao, wanashtumiwa kushiriki moja kwa moja katika mauaji ya mamia au hata maelfu ya Watutsi mwezi Aprili 1994 katika wilaya ya Kabarondo, hasa wakimbizi wa ndani walio kuwa walikusanyika katika kanisa wilayani humo, Mashariki mwa Rwanda, kwenye mpaka na Tanzania.

Wawili hawa, ambao walipishana katika uongozi wa wilaya hii, watasikilizwa kwa muda wa wiki nane kwa "uhalifu dhidi ya ubinadamu" na "mauaji ya kimbari", kwa "kitendo kilichotekelezwa kwa watu wengina kwa muda mfupi" katika "utekelezaji wa mpango wenye nia ya kuangamiza" kabila zima la Watutsi.

Kesi ya mauaji ya kimbari inawekwa wazi sasa nchini Ufaransa: katika wilaya ya Kabarondo, mauaji yalimalizika kabla ya mwisho wa mwezi Aprili, baada ya waasi wa Kitutsi wa Rwanda Patriotic Front (RPF, kwa sasa madarakani) kuingia nchini humo. Wakati ambapo mauaji ya kimbari yaliyogharimu maisha ya watu wasiopungua 800,000, yalilizika mwezi Julai mjini Kigali.

Siku thelathini za kusikilizwa, vifungo 31 vya utaratibu na mashahidi wasiopungua 90 kwa muda wa wiki nane vyote hivyo vitakua vimekamilisha kesi hiyo. Kesi hii ni ngumu kutokana na kuzorota kwa afya ya Tito Barahira, ambaye atatimiza umri wa miaka 65 mwezi Juni, na ambaye anahudumiwa kimatibabu mara tatu kwa wiki.

Kwa sababu hiyo, kesi hiyo itakua ikifupishwa kila Jumatatu na Jumatano. "itabidi kesi hii ifupishwe mara kwa mara. "Mteja wangu anahitaji mara kwa mara kuhudumiwa kimatibabu na kujinyoosha sakafuni," alionya Bw Philippe Meilhac, mwanasheria wa Tito Barahira.

Mamia ya mashahidi wanatarajiwa kusikilizwa katika kesi hii, miongoni mwao, kuhani wa Parukia ya Kabarondo, ambaye alishuhudia mauaji ya mamia ya watu kutoka jamii ya Watutsi ndani ya Kanisa lake. Kuhani huyo atasikilizwa ndani ya siku 15 zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.