Pata taarifa kuu
RWANDA-KUMBUKUMBU-MAUAJI

Uzinduzi wa wiki ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari Rwanda

Alhamisi hii Aprili 7, Rwanda inaadhimisha miaka 22 ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini humo mwaka 1994. Watu zaidi ya laki nane kutoka jamii ya Watutsi ikiwa ni pamoja na Wahutu wa msimamo wa wastani waliokua hawakubaliani na itikadi za Wahutu wenye msimamo mkali hasa chama cha MRND waliuawa.

Nchini Rwanda, moto wa kumbukumbu uliwashwa na Rais Kagame mwaka 2004 kwa kuadhimisha miaka 10 ya mauaji ya kimbari.
Nchini Rwanda, moto wa kumbukumbu uliwashwa na Rais Kagame mwaka 2004 kwa kuadhimisha miaka 10 ya mauaji ya kimbari. AFP PHOTO STR
Matangazo ya kibiashara

Chama cha MRND kilikua chama tawala wakati huo, kikiwa na wanamgambo waliojulikana kwa jina la INTERAHAMWE ambao walihusika katika mauaji hayo.

Mauaji hayo yalitokea baada ya kifo cha rais Juvenal Habyarimana, ambaye alikua aliambatana na mwenzake wa Burundi, Cyprien Ntaryamira, usiku wa tarehe 6 kuamkia 7 Aprili mwaka 1994.

Rais wa Tanzania John Magufuli, akizungumza mara baada ya kutembelea jumba la makumbusho ya mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994, amesema amesikitishwa na mauaji hayo, huku akionya kuwa mauaji ya kimbari sawa na yaliyotokea nchini Rwanda hayapswi kuruhusiwa kutokea tena.

"Haitatokea tena, hatuwezi kubadilisha yaliyopita lakini tunaweza kubadilisha mambo ya sasa na yajayo, mauaji haya hayapaswi kutokea tena," amesema Rais Magufuli, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.

Akihutubu wakati wa maadhimisho mafupi ya kukumbuka ya mauaji hayo, Mkuu wa kitengo cha kupambana na mauaji ya kimbari nchini Rwanda Jean Damascene Bizimana, amezihimiza nchi za Afrika Mashariki zinapaswa kubuni sheria za kufwatilia na kuwadhibiti watu wanaoeneza itikadi za mauaji ya kimbari.

Jean Damascene Bizimana amezinyooshea kidole cha lawama nchi za Burundi na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwapa hifadhi na kushirikiana na wapiganaji wa kundi la waasi wa Kihuru wa Rwanda (FDLR), wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji hayo.

Baada ya sherehe hiyo ya uzinduzi wa wiki ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Rais John Pombe Magufuli ameondoka Rwanda na kurejea nchi mwake.

Itafahamika kwamba Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Paul Kagame, Jumatano wiki hii, walifanya uzinduzi wa daraja la Rusumo linalounganisha Tanzania na Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.