Pata taarifa kuu
RWANDA-TANZANIA-USHIRIKIANO

Tanzania na Rwanda zaungana kwa maslahi ya wananchi wao

Baada ya kipindi fulani cha hali ya sintofahamu kati ya Rwanda na Tanzania, hatimaye nchi hizi mbili zimefungua ukurasa mpya, baada ya Marais wa nchi hizi kukutana Jumatano hii, nchini Rwanda.

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mwenyeji wake wa Rwanda Paul Kagame katika uzinduzi wa daraja la Rusumo.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mwenyeji wake wa Rwanda Paul Kagame katika uzinduzi wa daraja la Rusumo. YOUTUBE
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizi mbili zimeahidi kushirikiana zaidi katika kibiashara.

Hayo yanajiri wakati ambapo Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli yuko ziarani nchini Rwanda, ikiwa ni ziara yake ya kwanza nje ya nchi, tangu alipochukua hatamu ya uongozi wa nchi mwezi Oktoba mwaka jana.

Katika mkutano wa pamoja, Rais John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Bw Paul Kagame, wamesema " kunahitajika ushirikiano zaidi wa kibiashara baina ya mataifa haya mawili jirani."

Maneno ya kuonyesha na kukuza udugu, urafiki, uhusiano mwema na imara yamezungumziwa mara kadhaa na Marais hawa.

Rais Kagame amesema “mambo matatu ikiwa ni pamoja na udugu, urafiki na uhusiano mwema na imara ni msingi mkubwa wa ujenzi nchi hizi mbili”.

"Nimetekeleza mwaliko wa ndugu yangu Kagame”

Rais Magufuli amesema alialikwa kutembelea nchi nyingi, lakini hajafanya hivyo akibaini kwamba ni kutokana na sera yake ya "kubana matumizi".

''Nimealikwa kutembelea nchi nyingi, bado sijafanya hivyo. Lakini nilipoalikwa na ndugu yangu Rais Kagame tayari nimetekeleza hilo, na ndo maana nipo hapa, '' amesema Rais Magufuli.

Alhamisi hii, Aprili 7, Rais Magufuli ataungana na wananchi wa Rwanda katika maadhimisho ya miaka 22 ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari na baadaye atakutana na wandishi wa habari akiwa pamoja na Rais Paul Kagame.

Itafahamika kwamba Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Paul Kagame, Jumatano hii, wamefanya uzinduzi wa daraja la Rusumo linalounganisha Tanzania na Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.