Pata taarifa kuu
RWANDA-TANZANIA-MAUAJI-USHIRIKIANO

Rwanda kuadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya kimbari

Rwanda inaadhimisha kuanzia Jumatano hii jioni miaka 22 ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari, yaliyotokea nchini humo mwaka 1994, baada ya kifo cha rais Juvenal Habyarimana, ambaye alikua aliambatana na mwenzake wa Burundi, Cyprien Ntaryamira.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwasha moto wa ukumbusho katika eneo la kumbukumbu ya mauaji ya kimbari mjini Kigali, wakati wa maadhimisho ya miaka 21 ya mauaji ya kimbari, Aprili 7, 2015.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwasha moto wa ukumbusho katika eneo la kumbukumbu ya mauaji ya kimbari mjini Kigali, wakati wa maadhimisho ya miaka 21 ya mauaji ya kimbari, Aprili 7, 2015. AFP/StΓ©phanie Aglietti
Matangazo ya kibiashara

Lakini Sherehe rasmi zitafanyika Alhamisi hii katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Watu wasiopungua laki nane kutoka jamii za Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliouawa na utawala wa hayati rais Habyarimana baada ya ndege aliokuwemo kudunguliwa katika anga ya uwanja wa ndege wa Kanombe mjini Kigali usiku wa tarehe 6 kuamkia 7 Aprili 1994. Wanamgambo wa Kihutu wa INTERAHAMWE kutoka chama madarakani wakati huo cha MRND, chama cha rais Habyarimana walijihusisha na mauaji hayo ambayo baadhi ya wadadisi wanasema yalikua yalipangwa tangu kitambo.

Viongozi mbalimbali kutoka ukanda huu wanatazamia kuhudhuria sherehe hizi. Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli anatazamia kufanya ziara ya siku mbili nchini Rwanda kuanzia Jumatano hii Aprili 6, ambapo katika ziara hiyo atatembelea eneo la kumbukumbu la mauaji ya kimbari. Hii ni ziara ya kwanza ya nje ya Rais John Pombe Magufuli tangu alipochukua hatamu ya uongozi wa nchi mwezi Oktoba mwaka 2015.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania, Marais Magufuli na Kagame watafungua daraja la kimataifa la Rusumo na kituo cha huduma za pamoja katika mpaka wa Tanzania na Rwanda.

Kisha wataelekea Kigali ambapo watafanya mazungumzo ya pamoja. Bw Magufuli pia ataweka shada la maua katika makumbusho ya mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania, Rais Magufuli anafanya ziara hii nchini Rwanda baada ya kualikwa na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame.

Itakumbukwa kwamba Rais kagame amekua akimpokeza mweziye wa Tanzania kwa juhudi zake na kukabiliana na ufisadi ambao umekithiri katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Hivi karibuni Rais Kagame alisema kuwa anataka kumuiga mwenzake wa Tanzania kwa kukabiliana na mafisadi pamonja na kuinua uchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.