Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA-MAUAJI-SHERIA-HAKI

Mauaji ya kimbari: kesi ya Munyeshyaka yaombwa kufutwa

Mwendesha mashitaka wa mji wa Paris amepinga uamzi wa kumfikisha mahakamani Kasisi Wenceslas Munyeshyaka. Mwendesha mashitaka huyo ameomba Jumatano wiki hii kutokuwepo kwa uchunguzi wa kesi hii iliyofunguliwa tangu miaka 20 iliopita.

Akiwa na umri wa miaka 35, Wenceslas Munyeshyaka (kushoto) alikuwa Kuhani wa Parokia Sainte Famille mjini Kigali, wakati wa mauaji hayo. Hapa ni Juni 28, mwaka 1994, akiwa pamoja na mwanajeshi wa Rwanda.
Akiwa na umri wa miaka 35, Wenceslas Munyeshyaka (kushoto) alikuwa Kuhani wa Parokia Sainte Famille mjini Kigali, wakati wa mauaji hayo. Hapa ni Juni 28, mwaka 1994, akiwa pamoja na mwanajeshi wa Rwanda. AFP PHOTO / PIERRE BOUSSEL
Matangazo ya kibiashara

Kasisi huyo wa Rwanda anatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya kimbari yaliotokea nchini Rwanda mwaka 1994. Kasisi Munyeshyaka alikamatwa na kufanyiwa uchungu, wakati alipokimbilia nchini Ufaransa mwaka 1995.

Kazi kubwa kwa sasa inawasubiri majaji iwapo wataamua kwenda kinyume na ombi hilo la Mwendesha mashitaka na kuomba kesi hiyo isikilizwe.

Mwendesha mashitaka Paris alitumia umakini kwa kutoa maneno yake . " Jukumu la Wenceslas Munyeshyaka wakati wa mauaji hayo mwaka 1994 liliweza kuzua maswali mengi, lakini uchunguzi haukuruhusu ushirikiano wa kutosha ili kujua iwapo padiri Munyeshyaka alishiriki au la katika mauaji ya kimbari ", Mwendesha ameandika katika taarifa yake. Kwa hiyo kesi hiyo haihitajiki kusikilizwa baada ya kufunguliwa tangu miaka 20 iliopita.

Kesi ya Kasisi Munyeshyaka ilifunguliwa mwaka 1995, na januari mwaka 2012 ilikabidhiwa majaji ikiwa na tuhuma za "uhalifu dhidi ya ubinadamu". Tangu wakati huo mamia ya mashahidi wamesikilizwa, ili kujaribu kuamua bila upendeleo kuhusika au la kwa kasisi huyo wa Rwanda, ambaye alishtakiwa kwa mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Majaji ndio wanatakiwa kutoa uamzi

Wenceslas Munyeshyaka anatuhumiwa kuwa alisaidia wanamgambo wa Interahamwe kuwaua watu kutoka jamii ya Watutsi waliokimbilia katika kanisa lake mjini Kigali. Anatuhumiwa pia kuwabaka wanawake kutoka jamii hiyo ya Watutsi ndani ya kanisa ya kanisa lake.

Upande wa mashtaka na upande wa utetezi wamepewa mwezi mmoja kuwasilisha maoni yao kwa majaji wanaoendesha uchunguzi. Majaji hao hatimaye wataamua kama Wenceslas Munyeshyaka atafikishwa mahakamani au la.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.