Pata taarifa kuu

Tanzania yatia saini mikataba ya miradi ya ardhi adimu na grafiti

Tanzania imetia saini mikataba ya dola milioni 667 na makampuni ya Australia kuchimba madini adimu na grafiti. Mikataba hii inaonyesha nia ya serikali ya kuharakisha mazungumzo kuhusu miradi ya madini na nishati iliyosubiriwa kwa muda mrefu.

Kulingana na utafiti wa UNESCO, barafu katika maeneo yote ya Urithi wa Dunia barani Afrika itakuwa karibu kutoweka ifikapo mwaka 2050, ikiwa ni pamoja na Hifadhi ya Kitaifa ya Kilimanjaro na Mlima Kenya.
Kulingana na utafiti wa UNESCO, barafu katika maeneo yote ya Urithi wa Dunia barani Afrika itakuwa karibu kutoweka ifikapo mwaka 2050, ikiwa ni pamoja na Hifadhi ya Kitaifa ya Kilimanjaro na Mlima Kenya. © AP/Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Mikataba hii inahusisha makampuni ya Evolution Energy Minerals EV1.AX, Ecograf Ltd EGR.AX na Peak Rare Earths PEK.AX. Tanzania itamiliki asilimia 16 ya hisa kila moja katika makampuni yaliyoanzishwa kwa pamoja kuendesha miradi hiyo, amesema Palamagamba Kabudi, mwenyekiti wa timu ya mazungumzo.

Serikali ya Marekani na washirika wake, ikiwa ni pamoja na Australia, ambayo ina baadhi ya wazalishaji wakubwa zaidi wa ardhi adimu nje ya China, wanajitahidi kupunguza utegemezi wao kwa China.

Ardhi adimu ni kundi la madini 17 yanayotumika katika vifaa vya kielektroniki, magari ya umeme, simu janja, nishati mbadala na vifaa vya kijeshi.

Kama sehemu ya makubaliano na Peak Rare Earths, madini hayo yatachimbwa kusini magharibi mwa nchi huko Ngualla.

Palamagamba Kabudi anashikilia kuwa makampuni ya Evolution Energy Minerals na Ecograf yatachimba graphiti kusini na mashariki mwa Tanzania. Ecograf pia itachimba madini hayo kaskazini.

Grafiti ni madini yanayotumika kwa mwisho hasi (-) wa betri ya lithiamu-ioni, inayojulikana kama anode. Takriban 70% ya grafiti zote hutoka China na kuna mbadala chache zinazowezekana za betri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.