Pata taarifa kuu

Tanzania: Vitabu kinyume na 'viwango vya maadili' vyapigwa marufuku shuleni

Serikali ya Tanzania imepiga marufuku vitabu vingi vya watoto shuleni, hasa vya elimu ya ngono na vinavyoshutumu kwa kukiuka "kanuni za kitamaduni na maadili" za nchi hii ya Afrika Mashariki ambapo ushoga ni uhalifu.

Wasichana wa shule huko Kilolo, kilomita 500 kutoka Dar es Salaam, mji mkuu wa kiuchumi wa Tanzania. (Picha ya zamani)
Wasichana wa shule huko Kilolo, kilomita 500 kutoka Dar es Salaam, mji mkuu wa kiuchumi wa Tanzania. (Picha ya zamani) AFP - TONY KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

"Tunapiga marufuku vitabu hivi shuleni na miundo mingine ya kielimu kwa sababu ni kinyume cha kitamaduni na maadili," Waziri wa Elimu Adolf Mkenda aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu kutoka mji mkuu Dodoma.

Hasa, vitabu mbalimbali vya "Diary of a Wimpy Kid: Logbook by Greg Heffley", mfululizo wa vitabu vya Marekani vilivyo na picha ambavyo vimeuza mamilioni ya nakala duniani kote, vimepigwa marufuku mara moja.

Serikali haikusema ni kwa nini inalilenga 'gazeti' hili lililo na picha ya kijana, lakini ilisema ukaguzi ulifanywa katika maktaba za shule za umma na za kibinafsi ili kuhakikisha kuwa limeondolewa.

Waziri pia alijumuisha katika orodha hii ya kwanza ya vitabu "visivyokubalika" kitabu cha kiada kuhusu elimu ya ngono na vitabu vinavyotaja jamii ya wapenzi wa jinsia moja, LGBTQ.

Wiki iliyopita, rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliwataka viongozi wa wanafunzi kuwa makini na "tamaduni zinazoingizwa" kutoka nje ya nchi. "Kama wewe ni Mtanzania, ishi kulingana na tamaduni zetu," aliwaambia. Nchini Tanzania, ushoga unaadhibiwa kwa kifungo cha chini cha miaka 30 na hadi kifungo cha maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.