Pata taarifa kuu
TANZANIA- UKRAINE-URUSI

Tanzania yadhibitisha raia wake aliuawa Ukraine

Serikali ya Tanzania, imethibitisha kuwa raia wake kwa jina la Nemes Tarimo, aliyekuwa anasomea nchini Urusi, aliuawa mwaka uliopta katika vita vya Ukraine, akiwa anapigania Urusi kupitia kundi lake la Wagner.

Kundi la Wagner nchini Urusi
Kundi la Wagner nchini Urusi REUTERS - IGOR RUSSAK
Matangazo ya kibiashara

Dokta Stergomena Tax ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

“Taarifa tulizozipokea ni kwamba mwezi Machi mwaka wa 2022, Mtazania wetu huyu alihukumiwa kifo cha miaka saba kwa mujibu wa sheria za Urusi kwa vitendo vya uhalifu.”ameeleza Dokta Stergomena Tax.

Ripoti zinasema mwili wa Mtanzania huyo umesafirishwa nyumbani kwa ajili ya mazishi.

Mwaka uliopita, raia mwingine wa Zambia, aliyekuwa mwanafunzi aliuawa katika mazingira hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.