Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

CENI: Zaidi ya wapiga kura milioni 12 wamesajiliwa Magharibi mwa DRC

Nchini DRC, Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI) imefanya tathmini ya uandikishaji wa wapigakura katika uchaguzi wa Desemba 20, 2023. Kulingana na CENI, zoezi hili linakwenda vizuri

Makao makuu ya CENI, Tume ya Uchaguzi, mjini Kinshasa, DRC, Januari 9, 2019.
Makao makuu ya CENI, Tume ya Uchaguzi, mjini Kinshasa, DRC, Januari 9, 2019. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Kwa ukanda wa kwanza wa uendeshaji, unaohusu magharibi mwa nchi, na ambao shughuli zake zilianza Desemba 24, 2022, hadi Februari 8, zaidi ya wapiga kura milioni 12 wamesajiliwa: sawa na 64.35% ya zaidi ya milioni 18 inayotarajiwa. Kama ukumbusho, mnamo Januari 23, takwimu hii ilikuwa 37% tu.

Kwa eneo la pili, ambapo shughuli zimekuwa zikiendelea tangu Januari 25, 8% ya wapiga kura milioni 15 walikwenda kwenye vituo vya uandikishaji. Operesheni zinapaswa kuendelea angalau hadi Februari 23, lakini zinaweza kuongezwa kama ilivyokuwa kwa eneo la kwanza.

Hatimaye, ni Februari 16 ambapo uandikishaji utaanza katika eneo la tatu ambalo linahusu hasa maeneo yenye migogoro mashariki mwa nchi, ikiwa ni pamoja na mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.