Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

DRC: Waandamanaji 3 wauawa katika shambulio dhidi ya msafara MONUSCO

Waandamanaji watatu waliuawa mapema Jumanne jioni katika "shambulio kali" dhidi ya msafara wa Umoja wa Mataifa kilomita 2 kutoka Munigi, katikamkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kimesema kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) katika taarifa iliyowekwa kwenye Twitter.

Wanajeshi wa kikosi cha Umoja w Mataifa nchini DRC, MONUSCO, waliotumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Wanajeshi wa kikosi cha Umoja w Mataifa nchini DRC, MONUSCO, waliotumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. REUTERS - DJAFFAR SABITI
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kulazimisha msafara huo kusimama, "wavamizi" walichoma moto lori nne, "kabla ya kuiba mizigo ambayo lori hizo zilikuwa zikisheheni".

"Watu watatu kwa bahati mbaya walipoteza maisha wakati wa mapigano hayo", wakati walinda amani, ambao walikuwa wameandamana na askari wa Kongo, "walipojaribu kulinda msafara", taarifa hiyo inabainisha.

Wanajeshi wa MONUSCO walikuwa zwakirudi kutoka kwa misheni yao huko Kiwanja na walikuwa wakienda Goma, wakisindikizwa na jwanajeshi wa DRC, FARDC, MONUSCO imebainisha.

Kwa mujibu wa Jean-Claude Mambo Kawaya, kiongozi wa shirika moja la kiraia kwenye eneo la Nyiragongo, ambako shambulio hili limetokea, amesema lilijiri jirani na mji wa Kanyaruchinya, ambako maelfu ya raia wanaishi kwenye makambi.

Baada ya magari ya MONUSCO kuchomwa moto, baadhi ya waandamanaji walijaribu kufungua kontena lililokuwa na silaha hali iliyowafanya walinda amani kufyatua risasi na kuua watu watano, alisema mwanaharakati huyo.

"Raia na wakimbizi walishambulia msafara wa MONUSCO," alisema kanali Patrick Iduma, kiongozi wa eneo hilo bila hata hivyo kutoa taarifa zaidi.

Haya yanajiri wakati ambapo MONUSCO imekuwa ikikosolewa kwa kushindwa kuzuia machafuko yanayoendelea kwenye eneo la mashariki, na tangu wakati huo maandamano dhidi ya vikosi hivyo yameongezeka.

Mwezi Julai mwaka jana, waandamanaji walivamia kambi ya MOUSCO mjini GOma, Butembo na Beni pamoja na maeneo mengine, wakishinikiwa walinda amani hao kuondoka, ambapo watu 36 waliuawa, wakiwemo wanajeshi 4.

Siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita, wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, walitaka usitishwaji mara moja wa mapigano mashariki mwa DRC, wakati wa kikao chao cha dharura kilichofanyika mjini Bujumbura, Burundi.

Juma hili mwanajeshi mmoja wa Afrika Kusini aliuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya siku ya Jumapili, wakati ndege yao aina ya Helikopta, iliposhambuliwa kwa risasi jimboni Kivu Kaskazini.

Mwezi Machi mwaka jana, walinda amani 8 waliuawa wakati helikopta yao ilipoanguka jirani na eneo kulikokuwa na mapigano kati ya wanajeshi wa Serikali FARDC na waasi wa M23.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.