Pata taarifa kuu
DRC - USALAMA

DRC: UN yarekebisha takwimu za mauaji huko Kishishe hadi watu 171

Ofisi ya Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za binadamu katika ripoti yake mpya kuhusu hali ya haki za binadamu nchini DRC, inasema idadi ya raia waliouawa katika kijiji cha Kishishe na Bambo, jimboni Kivu Kaskazini mwezi Novemba mwaka ulioipita, ni 171 na sio 131 kama ilivyoripoti hapo awali.

Wapiganaji wa M23, Mashariki mwa DRC.
REUTERS/James Akena (DEMOCRATIC REPUBLIC OF CONGO - Tags: CIVIL UNREST POLITICS)
Wapiganaji wa M23, Mashariki mwa DRC. REUTERS/James Akena (DEMOCRATIC REPUBLIC OF CONGO - Tags: CIVIL UNREST POLITICS) REUTERS - JAMES AKENA
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake, inayoeleza mukhtasari wa matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini DRC mwaka uliopita, imetoa takwimu hizi mpya baada ya uchunguzi wa kina kufanyika.

Mauaji hayo, yalizua hasira kwa wakaazi na serikali ya Kinshasa, ambayo ilisema waasi hao waliwaua watu zaidi ya 300 huku M23 ikikanusha shutuma za kuhusika na mauaji hayo, na kujitetea kuwa waliwaua raia wanane kwa kuwapiga risasi kwa bahati mbaya.

Siku ya Jumatatu, Shirika la Kimataifa la Kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, katika ripoti yake, liliwashtumu waasi wa M23 kwa kuwanyonga watu 22 kijijini Kishishe na kuwaua wengine 10.

Mkuu wa Human Rights Watch barani Afrika Thomas Fessy, amesema wameorodhesha mauaji ya pamoja lakini pia kusajiliwa kwa vijana katika shughuli za kijeshi.

Mfano Oktoba 28, waasi wa M23 walifyatulia risasi basi la abiria, na pikipiki mbili juu yake watu waliokuwa wakikimbia mapigano karibu na mji wa Lugari. Amesema Fessy.

Katika hatua nyingine, Umoja wa Mataifa unasema, visa zaidi ya Elfu Sita vya ukiukwaji wa haki za binadamu, viliripotiwa nchini DRC ikiwa ni punguzo la asilimia 15 ikilinganishwa na mwaka 2021.

Makundi ya waasi ya M23, Codeco, Nyatura na ADF wametajwa kuendeleza visa hivyo vya ukiukwaji wa haki za binadamu hasa mauaji, ubakaji na utekaji wa raia.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.