Pata taarifa kuu
DRC - USALAMA

DRC: HWR yasema M23 inachochea mgawanyiko wa kikabila

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch, limesema kundi la waasi la M23, linaloungwa mkono na nchi ya Rwanda, linachochea mgawanyiko wa kikabila nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

HRW yaonya kuhusu M23 kuchochea kabila la Tutsi na Hutu nchini DRC
 @HRW
HRW yaonya kuhusu M23 kuchochea kabila la Tutsi na Hutu nchini DRC @HRW © HRW
Matangazo ya kibiashara

HRW imeonya kuhusu kuongezeka kwa mvutano kati ya makabila ya Watutsi na Wahutu mashariki mwa DRC, kutokana na mapigano yanayohusisha kundi la waasi wa M23, ambalo limekuwa likitekeleza mauaji pamoja na kuwasajili raia kwa lazima.

Shirika hilo piza limesema kundi hilo la waasi limekuwa likicha nyuma ushahidi wa matukio ya uhalifu wa kivita, HRW sasa likitaka msaada wowote wa kijeshi kwa nchi ya Rwanda kusitishwa.

Katika hatua nyingine, shirika hilo limesema, jeshi la congo limekuwa likifanya kazi na makundi mbalimbali yenye silaha, likiwemo kundi la Hutu lenye historia ya kutekeleza unyanyasaji.

Serikali ya Kinshasa, imeendelea kuituhumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23, madai ambayo Rwanda inakanusha.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.