Pata taarifa kuu
DRC

Wakaazi wa Sake wayakimbia makwao kufuatia mapigano kati ya M 23 na wanajeshi wa DRC

Mapigano makali yameripotiwa kati ya Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M 23 katika kijiji cha Luhonga, karibu na mji wa Sake, jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa nchi hiyo.

Wakaazi wa Sake wakikimbia mapigano kati ya M 23 na wanajeshi wa FARDC
Wakaazi wa Sake wakikimbia mapigano kati ya M 23 na wanajeshi wa FARDC © Benjamin Kasembe
Matangazo ya kibiashara

Mwandishi wetu wa Goma Benjamin Kasembe, aliyezuru  mji wa Sake, alikutana na mamia ya watu wakiyakimbia makwao, kwa kuhofia maisha yao wakielekea Goma, Minova huku wengine wakishika barabara ya kwenda Bukavu.

“Hali ni ya wasiwasi, milio ya risasi inasikika, raia wanakimbia,” Kasembe aliiambia RFI Kiswahili akiwa mjii Goma.

Mapigano haya yanakuja baada ya waasi wa M 23 kuudhibiti mji wa kimkakati wa Kitchanga, na kuongeza wasiwasi kuwa huenda wakafika mjini Goma katika siku zijazo.

Tangu mwaka uliopita, mapigano kati ya waasi wa M 23 yameendelea kushuhudiwa licha ya kuwepo kwa mikutano ya viongozi wa kikanda jijini Luanda nchini Angola na Nairobi nchini Kenya, kuyataka makundi ya waasi kuweka silaha nchini na kuacha mapigano.

Mwezi Novemba mwaka uliopita, kikosi cha pamoja cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kilitumwa Mashariki mwa DRC kusaidia kuleta amani, lakini pia uwepo wa jeshi hilo haujazaa matunda makubwa.

Wiki hii, wakaazi wa Goma waliandamana kushinikiza kundoka kwa vikosi vya Jumuiya hiyo na vile vya Umoja wa Mataifa MONUSCO kwa madai ya kushinda kukabiliana na kundi la M 23 na makundi mengine ya waasi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.