Pata taarifa kuu

DRC: Rais Tshisekedi awashawishi wawekezaji kuhusu kuboreka kwa mazingira ya biashara DRC

"Mining Indaba", mkutano mkuu wa kila mwaka kuhusu sekta ya madini barani Afrika, unafanyika wiki nzima mjini Cape Town (Afrika Kusini). Mwaka huu, metali za mpito kwa aina mpya za nishati ziko katika uangalizi, wakati mataifa yenye nguvu duniani yanajaribu kuhakikisha usalama wao wa nishati ya baadaye. 

Rais wa DRC Félix Tshisekedi, hapa wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa, Novemba 21, 2022.
Rais wa DRC Félix Tshisekedi, hapa wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa, Novemba 21, 2022. © Arsène Mpiana / AFP
Matangazo ya kibiashara

DRC, ikiwa na akiba yake kubwa sana, inatarajia kufanya vyema.Rais Félix Tshisekedi amefanya ziara nchini Afrika Kusini ili kuwashawishi wawekezaji kufikirianchi yake, licha ya ukosefu wa usalama Mashariki mwa nchi.

Kulingana na Rais wa DRC, Félix Tshisekedi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) "iko tayari kutekeleza sehemu yake" katika mpito wa nishati, na kuwa "mahali pa chaguo barani Afrika", kutokana na rasilimali muhimu.

Mzalishaji mkubwa zaidi duniani wa cobalt, nchi hiyo pia ina ardhi yenye akiba ya shaba na ambayo haijatumika ya lithiamu, madini muhimu kwa ajili ya utengenezaji, hasa, wa betri za magari ya umeme.

Mbali na utumiaji rahisi, Kinshasa pia inatarajia kupata ufadhili wa kuendeleza mabadiliko ya madini yake muhimu, ili kunufaika zaidi na utajiri wake, ikiwa imesalia mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa urais, uliopangwa kufanyika mwezi Desemba 2023.

Félix Tshisekedi kwa hiyo amejaribu kuwashawishi wawekezaji kuhusu kuboreka kwa mazingira ya biashara na matarajio ya uchimbaji madini ya DRC,mbali na hatari za usalama mashariki mwa nchi hiyo, pamoja na mambo mengine, mapigano kati ya jeshi na waasi wa M23. Uasi ambao, kulingana na mkuu wa nchi, "yanayochochewa na jirani yake, Rwanda, ikilenga utajiri (wetu)".

Operesheni ya kuwashawishi Wakongo lazima iendelee Jumatano hii, Februari 8. Kiamsha kinywa kimeandaliwa ili kutangaza vivutio vya Kinshasa kwa wawekezaji wa madini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.