Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Umoja wa Mataifa: Maelfu ya watu wayakimia makazi yao kufuatia mapigano mapya Upper Nile

Umoja wa Mataifa unasema watu karibu Elfu 40, wameyakimbia makaazi yao, kufuatia mapigano mapya yanayoendelea katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la  Upper Nile nchini Sudan Kusini.

Raia wa Sudan Kusini wakimbia mapigano huko Malakal siku ya Alhamisi (tarehe 18 Februari) baada ya watu wenye silaha kuwafyatulia risasi raia katika kambi ya Umoja wa Mataifa.
Raia wa Sudan Kusini wakimbia mapigano huko Malakal siku ya Alhamisi (tarehe 18 Februari) baada ya watu wenye silaha kuwafyatulia risasi raia katika kambi ya Umoja wa Mataifa. Justin LYNCH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake ya hivi punde, Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia misaada ya kibinadamu OCHA, mapigano yanayoendelea pia yanarudisha nyuma jitihada za kuwasaidia, watu hao wanaokimbia katika jimbo hilo. 

Aidha, OCHA inasema watu hao wanaoshi katika mazingira, na wanahitaji msaada wa haraka, ili kuokoa maisha yao. 

Wiki iliypita, watalaam wanaoshughulikia usitshwaji wa vita vya mara kwa mara, walisema wangezuru katika êneo hilo kujionea na kuchunguza kwa kina zaidi mapigano hayo mapya. 

Tangu mwezi Novemba, mapigano yameripotiwa kati ya jeshi la taifa na kundi la wapiganaji wa upinzani linalojiita, Maiwut, katika êneo hilo ambalo pia limeendelea kushuhudia mapigano ya kikabila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.