Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI- SIASA

Sudan Kusini: Watu 40,000 wameyakimbia makazi yao kwa hofu ya kushambuliwa

Umoja wa Mataifa unasema watu karibu Elfu 40, wameyakimbia makaazi yao, kufuatia mapigano mapya yanayoendelea katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Upper Nile nchini Sudan Kusini.

Wakimbizi wa ndani wakiwa katika makazi ya muda nchini Sudani Kusini.
Wakimbizi wa ndani wakiwa katika makazi ya muda nchini Sudani Kusini. Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake ya hivi punde, Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia misaada ya kibinadamu OCHA, mapigano yanayoendelea pia yanarudisha nyuma jitihada za kuwasaidia, watu hao wanaokimbia katika jimbo hilo.

Aidha, OCHA inasema watu hao wanaoshi katika mazingira, na wanahitaji msaada wa haraka, ili kuokoa maisha yao.

Wiki iliypita, watalaam wanaoshughulikia usitshwaji wa vita vya mara kwa mara, walisema wangezuru katika eneo hilo kujionea na kuchunguza kwa kina zaidi mapigano hayo mapya.

Tangu mwezi Novemba, mapigano yameripotiwa kati ya jeshi la taifa na kundi la wapiganaji wa upinzani linalojiita, Maiwut, katika eneo hilo ambalo pia limeendelea kushuhudia mapigano ya kikabila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.