Pata taarifa kuu

Papa kuzuru DRC na Sudan Kusini kuanzia Januari 31 hadi Februari 5

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, atazuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kisha Sudan Kusini kuanzia Januari 31 hadi Februari 5, 2023, Vatican imetangaza Alhamisi Desema 1, 2022. Ziara hii ilipangwa awali msimu wa joto uliopita lakini iliahirishwa kwa sababu za kiafya.

Papa Francis mjini Vatican, Oktoba 23, 2022.
Papa Francis mjini Vatican, Oktoba 23, 2022. AP - Alessandra Tarantino
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Kanisa Katoliki kutoka Argentina atazuru Kinshasa kuanzia Januari 31 hadi Februari 3, 2023, kisha Juba kuanzia Februari 3 hadi 5, alisema mkurugenzi wa huduma ya vyombo vya habari wa makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Matteo Bruni, katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Akiwa ameshawishika na madaktari wake kuacha kufanya safari hii ndefu mwezi Julai kama ilivyopangwa kwa sababu ya matatizo yake ya goti, PapaFrancis hakukata tamaa ya kutembelea nchi hizi mbili za Afrika. Baada ya ziara yake nchini Canada, Kazakhstan na Bahrain, kwa hiyo ataweza kwenda Kinshasa na Juba, hatua kuu mbili za ziara hii ndogo. 

Siku ya Jumanne Januari 31, Papa ataondoka Roma kuelekea Kinshasa. Baada ya kuwasili, baada ya ziara ya heshima kwa Rais Tshisekedi, atakutana na mamlaka, mashirika ya kiraia na mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini DRC katika makao makuu ya Bunge na kutoa hotuba yake.

Siku inayofuata, Februari 1, ataadhimisha Misa katika uwanja wa ndege wa Ndolo asubuhi. Mchana, atakutana na waathiriwa wa vurugu mashariki mwa nchi na wawakilishi wa baadhi ya mashirika ya misaada, fursa kwake, kila wakati, kutoa hotuba.

Tarehe 2 Februari, mkutano kati ya Papa na vijana na makatekista umepangwa katika uwanja wa Martyrs. Mchana, atashiriki katika kanisa kuu la Notre-Dame-du-Congo katika mkutano wa maombi na mapadre.

Februari 3, kabla ya kuondoka DRC, atakutana na maaskofu wa Kongo kwenye makao makuu ya CENCO, Baraza Kuu la maaskofu wa nchi hiyo. Kisha atasafiri kwa ndege hadi Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, safari atakayofanya pamoja na Askofu Mkuu wa Canterbury na Msimamizi wa Baraza Kuu la Kanisa la Scotland.

Mchana, atakuwa na mahojiano na rais wa Sudan Kusini, na makamu wa rais. Atazungumza hadharani mbele ya mamlaka, mashirika ya kiraia na mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Sudan Kusini.

Jumamosi, Februari 4, Francis atazungumza na maaskofu, mapadre katika Kanisa Kuu la Sainte-Thérèse asubuhi, kabla ya kuwapokea kwa faragha Wajesuti wa nchi hiyo. Alasiri, atazungumza na watu waliohamishwa kabla ya kushiriki katika sala ya kiekumene katika Makaburi ya John Garang.

Jumapili, Februari 5, kabla ya kurudi Roma mchana, atahudhuria misa kwenye kaburi la John Garang.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.