Pata taarifa kuu

Sudan Kusini 'yasherehekea' kwa huzuni miaka minne ya makubaliano ya amani

Miaka minne baada ya kusainiwa, mkataba wa amani nchini Sudan Kusini, umeshindwa kuboresha maisha ya watu wengi wa nchi hiyo. Kati ya ukosefu wa utulivu na kutokujali kwa uhalifu wa kivita, hali bado ni ngumu.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, kiongozi wa upinzani Riek Machar na Mohamed Hamdan Daglo "Hemeti" baada ya mkutano wao na waandishi wa habari mjini Juba, Desemba 17, 2019.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, kiongozi wa upinzani Riek Machar na Mohamed Hamdan Daglo "Hemeti" baada ya mkutano wao na waandishi wa habari mjini Juba, Desemba 17, 2019. Majak Kuany / AFP
Matangazo ya kibiashara

Nchini Sudan Kusini, ni miaka minne ya mkataba wa amani "uliohuishwa", uliotiwa saini mwaka 2018 ili kumaliza vita vilivyoanza mwaka 2013. Makubaliano kati ya Rais Salva Kiir na makundi kadhaa ya upinzani, akiwemo makamu wa Rais Riek Machar, ambaye hakukuleta amani na utulivu vilivyotarajiwa na wananchi wa Sudan Kusini. Kipindi cha mpito ambacho kinafaa kuiongoza nchi kwenye uchaguzi kiliongezwa kwa miaka miwili mwanzoni mwa mwezi Agosti.

Maendeleo mengine ya hivi majuzi: kikosi cha kwanza cha vikosi vya umoja wa kijeshi kimeagizwa, kifungu kikuu cha makubaliano. Kwa watu wa Jimbo la Unity, eneo ambalo limekumbwa na migogoro licha ya makubaliano ya amani, haki kwa uhalifu uliotendwa na nia ya kisiasa ya kutekeleza makubaliano hayo kwa dhati ndivyo vinavyozingatiwa leo.

'Mkataba wa amani haujawahi kutangazwa'

Thor Youanes, mwanaharakati wa mashirika ya kiraia, anafanya kazi katika jimbo la Unity kusini anasema: "Kuna mchakato wa amani, lakini unajulikana tu huko Juba kwa sababu mkataba wa amani haujawahi kutangazwa. Kama wanaharakati, tunadai mtaba huo ufafanuliwe kwa wakazi wa eneo hili. »

amewanyooshea kidole cha lawama viongozi wa eneo hilo kwamba wanapuuza mchakato wa amani: “Jamii ya watu wa Jimbo la Unity Kusini imeishi kwa amani kwa karne nyingi. Lakini mapambano ya kuwania madaraka ya wanasiasa yameathiri na kugawanya watu wa eneo hilo. Migawanyiko ya kisiasa imeenea ndani ya jamii. Watu hawajui kama kuna amani. Wanachojua wao ni kwamba kuna vita kati ya serikali na upinzani, hadi leo. "

'Watu wanaishi katika mazingira magumu'

Nyakume Peter ni mwanaharakati kutoka Kaunti ya Leer, ambayo pia iliharibiwa na mapigano. Hata Umoja wa Mataifa ulishutumu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika ripoti ya hivi majuzi: “Watu wamekuwa wakilalamika na kuuliza, ‘mbona viongozi wetu hawawezi kwenda katika maeneo ya matukio kuona mateso ya watu wetu?’ Juba, wanafikiri kuna amani, lakini pia kuna maeneo haya ambayo watu wanateseka, ambapo watu wanaishi katika kambi, ambapo watu wanaishi kwa taabu kimaumbile, kwenye vinamasi”.

Kwake, haki kwa uhalifu uliotendwa ni sharti la kujenga amani ya kudumu katika eneo lake na nchi nzima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.