Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Umoja wa Mataifa: Raia 173 waliuawa katika kipindi cha miezi minne Sudan Kusini

Takriban raia 173 wameuawa na 37 kutekwa nyara katika kpindi cha miezi minne nchini Sudan Kusini katika mapigano kati ya vikosi vinavyomtii Rais Salva Kiir na vile vinavyomtii Makamu wa Rais Riek Machar, Umoja wa Mataifa umetangaza leo Jumanne, pia ukilaani visa vingi vya unyanyasaji wa kingono.

Wakati makundi ya pande zote mbili yanahusika katika ghasia hizo, vikosi vya serikali na wanamgambo watiifu kwa Rais Salva Kiir "wanahusika zaidi na ukiukwaji na uvunjaji wa haki za binadamu", kulingana na Umoja wa Mataifa.
Wakati makundi ya pande zote mbili yanahusika katika ghasia hizo, vikosi vya serikali na wanamgambo watiifu kwa Rais Salva Kiir "wanahusika zaidi na ukiukwaji na uvunjaji wa haki za binadamu", kulingana na Umoja wa Mataifa. REUTERS/UNMISS/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yalifanyika kati ya mwezi wa Februari na Mei katika kaunti za Koch, Leer na Mayendit, zilizoko takriban kilomita 400 kaskazini mwa mji mkuu Juba katika Jimbo la Unity, ngome ya vikosi vinavyomuunga mkono Machar, SPLA-IO.

"Mapigano katika Jimbo la Unity kusini yameathiri takriban vijiji 28 ... na inakadiriwa kuwa raia 173 wameuawa, 12 wamejeruhiwa na wanawake 37 na watoto kutekwa nyara", kulingana na ripoti ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini (UNMISS).

Baadhi ya watu waliotekwa nyara walikumbwa na "unyanyasaji wa kijinsia, wakiwemo wasichana wa umri wa miaka minane", kulingana na Umoja wa Mataifa. Msichana wa miaka tisa alikufa baada ya kubakwa na kundi la watu, kulingana na UNMISS, ambayo inasema imeorodhesha watu131 waliobakwa na wengine kubakwa na makundi ya wahalifu. Vurugu hizi pia zilisababisha takriban watu 44,000 kukimbia vijiji vyao.

Wakati makundi ya pande zote mbili yanahusika katika ghasia hizo, vikosi vya serikali na wanamgambo watiifu kwa Rais Salva Kiir "wanahusika zaidi na ukiukwaji na uvunjaji wa haki za binadamu", kulingana na Umoja wa Mataifa, ikimaanisha hasa mashambulizi "yaliyopangwa".

"Kwa kutokujali"

"Ukiukaji wa haki za binadamu umefanywa bila kuadhibiwa kabisa," amesema mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Nicholas Haysom. Kulingana na sheria za kimataifa, mamlaka lazima "zilinde raia, kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu unaoshukiwa," amekumbusha.

Tangu uhuru wake kutoka kwa Sudan mwaka 2011, Sudan Kusini imekuwa ikikumbwa na ghasia za kisiasa, za kikabila na ukosefu wa utulivu wa muda mrefu, ambao umeizuia kutoka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha umwagaji damu, ambavyo vilisababisha vifo vya karibu 400,000 na mamilioni ya watu kutoroka makazi yao kati ya mwaka 2013 na 2018.

Mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka wa 2018 unatoa kanuni ya kugawana madaraka ndani ya serikali ya umoja wa kitaifa, iliyoundwa Februari 2020 na Kiir kama rais na Machar kama makamu wa rais. Lakini kwa kiasi kikubwa ilibaki bila kutekelezwa, na kuacha nchi katika machafuko.

Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa mara kwa mara huwashutumu viongozi wa Sudan Kusini kwa kudumisha hali iliyopo, kuchochea ghasia, kukandamiza uhuru wa kisiasa na ubadhirifu wa fedha za umma.

Katikati ya mwezi Julai, Marekani ilijiondoa kutoka kwa walinzi wawili wa mchakato wa amani kutokana na "ukosefu wa maendeleo" katika mchakato wa mpito na "ukosefu wa nia ya kisiasa" ya viongozi wake kuleta amani nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.