Kundi jipya lateka Mayom Kaskazini mwa jiji la Juba
Nchini Sudan Kusini, kundi jipya la waasi limedhibiti Kaunti ya Mayom, Kaskazini mwa jiji kuu Juba, na kuzua hali ya wasiwasi, wakati huu nchi hiyo inapoendelea kukabiliwa na utovu wa usalama, tangu kutiwa saini kwa mkataba wa amani mwaka 2018.
Imechapishwa:
Kundi hilo ambalo linajiita People’s Army of South Sudan, linaongozwa na mwanajeshi aliyeasi katika jeshi la Sudan Kusini: Meja-Jenerali Steven Buoy Roinyang.
Niko kwenye uwanja wa mapigano hapa mayom. Tumeanzisha kundi jipya linalotambulikana kama South Sudan People’s Army, kwa njia nyingine South Sudan People’s Army. Tunalenga kuiangusha serikali iliyoko sasa ili tuwape wananchi wa Sudan kusini fursa ya kuwachagua viongozi wao katika uchaguzi huru na wa haki.
Waziri Wa Habari, Michael Makwei, alikataa kuzungumzia suala hilo na kumwachia Mkuu wa Majeshi aliyekuwa na kauli hii.
Wanajeshi wetu wameanzisha msako mkubwa ukiwa na madhumuni ya kumnasa kiongozi wa waasi. Hatua kali itachukuliwa. Atalipa gharama kubwa kutokana na uasi aliotekeleza.
Sudan Kusini ina makundi kumi ya waasi. Makundi manane yalisaini mkataba wa amani ambao ulileta serikali inayotawala sasa. Wanajeshi waasi tiifu kwa Meja-Jenerali Steven Buoy Roinyang, wanadhihirisha jinsi hali ilivyo ngumu ya kuimarisha amani nchini Sudan Kusini, miaka kumi-na-moja baada ya kutangazwa kama nchi huru.