Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI- SIASA

Sudan Kusini: Mazungumzo ya upatikanaji wa amani yarejelewa mjini Rome.

Mazungumzo ya amani kuhusu Sudan Kusini, yanayosimamiwa na kituo kimoja cha kanisa katoliki nchini Itali, yameanza tena mjini Rome, kujaribu kuyaunganisha makundi ya kisiasa ambayo yameendelea kugawanyika na kutishia upatikanaji wa suluhu ya kudumu kwenye taifa hilo.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na makamu wa rais Riek Machar
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na makamu wa rais Riek Machar AFP - PETER LOUIS GUME
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya yamerejelewa nchini Italia, yakiuhusisha serikali, chama cha SPLM kikiongozwa na katibu mkuu wake Pagan Amum, na kundi la upinzani la SSUF, likiongozwa na Jenerali Paul Malong;

Hata hivyo mazungumzo haya yameendelea bila kuhusisha makundi yaliyo na uhusiano na kundi la National Salvation Front (NAS), linaloongozwa na Jenerali Thomas Cirillo.

Lengo la kwanza la mchakato huu ni kuzishawishi pande husika kutekeleza kikamilifu mkataba wa 2017, ambao walisaini jijini Addis Ababa, Ethiopia, kabla ya waasi waliosalia kukataa makubaliano ya amani ya Septemba mwaka 2019.

Waitishaji wa mazungumzo haya kati ya serikali na upinzani nchini Sudan Kusini, wamelazimika kufanya vikao tofauti, kutokana na hali ya kusuasua ambayo imesababishwa na mgawanyiko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.