Pata taarifa kuu
UBAKAJI-HAKI

Mwanadiplomasia wa Sudan Kusini ashtakiwa kwa ubakaji mjini New York

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan Kusini imesema ilimsimamisha kazi na kumrudisha nyumbani mwanadiplomasia mmoja anayeishi Marekani ili kusubiri matokeo ya uchunguzi dhidi yake kwa tuhuma za ubakaji mjini New York.

Vyombo vya habari vya Marekani vimesema kuwa mwanamke mmoja alimshutumu kwa kuingia kwa nguvu katika nyumba yake ya Manhattan siku ya Jumapili na kumbaka.
Vyombo vya habari vya Marekani vimesema kuwa mwanamke mmoja alimshutumu kwa kuingia kwa nguvu katika nyumba yake ya Manhattan siku ya Jumapili na kumbaka. © CC0 Pixabay/Manuel Romero
Matangazo ya kibiashara

"Ni kwa masikitiko kwamba mwanadiplomasia wetu alihusika katika tukio la madai ya ubakaji na mkazi wa New York," Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imesema katika taarifa iliyochapishwa Alhamisi jioni kwenye ukurasa wa serikali wa Twitter.

"Mwanadiplomasia husika sasa amerejea nchini Sudan Kusini na amesimamishwa kazi, akisubiri matokeo ya uchunguzi huu," ilisema taarifa hiyo, ikiongeza "uhalifu wa kingono kwa namna yoyote ni wa kuchukiza na haukubaliki kabisa".

Aachiliwa kwa sababu ya kinga ya kidiplomasia

Taarifa hiyo haikubainisha aina ya mashtaka dhidi ya mwanadiplomasia huyo, lakini vyombo vya habari vya Marekani vimesema kuwa mwanamke mmoja alimshutumu kwa kuingia kwa nguvu katika nyumba yake ya Manhattan siku ya Jumapili na kumbaka. Alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi na maafisa wa polisi, ambao walimwachilia baada ya kudai kinga ya kidiplomasia.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema Jumatano kwamba "inafahamu tukio (...) linalohusisha mwanadiplomasia aliyeidhinishwa na Umoja wa Mataifa". "Tunachukulia madai haya kwa uzito mkubwa na tunafanya kazi kwa karibu na NYPD na ofisi ya meya wa masuala ya kimataifa," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Vedant Patel alisema.

Nchi changa zaidi duniani, Sudan Kusini ilipata kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa Julai 14, 2011, siku chache baada ya kujitangazia uhuru wake kutoka kwa Sudan Julai 9.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.