Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Jeshi la Uganda kuondoka DRC baada ya kukamilisha operesheni ya pamoja dhidi ya ADF

Jeshi la Uganda (UDF) linasema halitaondoka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hadi pale waasi wa ADF watakaposhindwa.

Vikosi vya usalama vya Uganda vilitumwa Kampala Novemba 16, 2021, saa chache baada ya milipuko miwili mbaya iliyodaixa na kundi la waasi la ADF.
Vikosi vya usalama vya Uganda vilitumwa Kampala Novemba 16, 2021, saa chache baada ya milipuko miwili mbaya iliyodaixa na kundi la waasi la ADF. © AP - Ronald Kabuubi
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi, wakaazi wa Mashariki mwa DRC wanasema walishuhudia wanajeshi wa Uganda na magari yakivuka mpaka wa Mobili kuingia nchini humo.

Katika hatua nyingine, mateka 28 wakiwemo wanawake watano waliokuwa wameshikiliwa na waasi wa ADF wamefanikiwa kutoroka katika eneo la Luna Etat, baada ya mashambulizi ya jeshi la Uganda dhidi ya waasi hao.

Operesheni za pamoja kati ya DRC na majeshi ya Uganda zinaendelea katika eneo la Beni, katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Mashambulizi ya anga na hatua za ardhini zinatekelezwa dhidi ya ngome za kundi la ADF, serikali na jeshi la DRC walithibitisha tangu Jumanne.

Kundi la waasi wa ADF linahusishwa katika mauaji na vitendo vya kikatili dhidi raia wa maeneo ya mpaka na Uganda, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, upande wa mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.