Pata taarifa kuu
UGANDA

Ifahamu Uganda inayoadhimisha miaka 59 ya uhuru wake

Uganda inaadhimisha miaka 59 ya uhuru hivi leo. Mwaka 1962 nchi hiyo ya Afrika Mashariki ilianza kujitawala baada ya kupata uhuru kutoka kwa wakoloni wa Uingereza.

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni. AP - John Muchucha
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, maadhimisho ya mwaka huu kama ilivyokuwa mwaka uliopita, yakuvutia umati mkubwa wa watu, kwa sababu ya janga la Covid 19.

Uganda ni nchi ya Afrika Mashariki na moja wa wasisi wa jumuiya ya Afrika mashariki. Inapakana na Sudan Kusini, Kenya, Tanzania, Rwanda, na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC). Ilipata uhuru wake mwaka 1962.

Uganda ni nchi isiyokuwa na mlango wa bahari na ambayo sura yake inajumlisha milima ya theluji ya Rwenzori na ziwa Victoria. Wanyamapori wake ni pamoja na masokwe wanaokabiliwa na kitisho cha kutoweka na nyani, na vile vile ndege adimu. Msitu mkubwa wa Bwindi ni maarufu kwa kuwahifadhi sokwe wa milimani, wakati mbuga ya wanyama ya Murchison Falls iliyoko kaskazini-magharibi inajulikana kwa maporomoko yake ya maji yenye urefu wa mita 43 na wanyamapori kama vile Kiboko. Mji wake mkuu ni Kampala, lakini miji mingine maarufu ni pamoja na Entebbe, unakapatikana uwanja wa ndege wa kimatafa, Jinja - mji uliyokuwa chemchem ya viwanda, Mbale, Masaka, Mbarara na mingine. Kama ilivyo kwa Tanzania na Kenya, sarafu ya Uganda ni shilingi.

Baada ya uhuru

Uganda ilipata uhuru wake tarehe 9 Oktoba 1962 kwa katiba ya jamhuri yenye serikali ya kibunge.

Rais wa kwanza alikuwa Kabaka Sir Edward Mutesa II na waziri mkuu Milton Obote.

Mwaka 1967 Obote alibadilisha katiba akamfukuza Kabaka nchini.

Serikali ya Obote ilipinduliwa na mkuu wa jeshi Idi Amini mwaka 1971. Utawala wake ulikuwa kipindi cha udikteta ulioharibu uchumi wa nchi na misingi ya dola. Takriban watu 300,000 waliuawa chini ya Amin ama wapinzani wa siasa zake ama watu wa makabila yaliyotazamiwa kuwa maadui wa serikali. Raia wenye asili ya Asia walifukuzwa katika nchi na mali yao yote kutwaliwa na serikali.

Mwaka 1978 vikosi vya jeshi la Uganda viliingia Tanzania na kuvamia maeneo ya mpakani kaskazini kwa mto Kagera. Mwaka 1979 Tanzania ilijibu njia ya vita na jeshi lake pamoja na wapinzani wa Uganda walinda jeshi la Amin na kumfukuza dikteta nchini. Rais wa baadaye Yoweri Museveni alikuwako kati ya wanamigambo waliosaidiana na Watanzania.

Uchaguzi wa mwaka 1980 ulimrudisha madarakani Milton Obote aliyeanzisha upya udikteta na kuua watu wako. Wapinzani wake wakiongozwa na Museveni walirudi porini wakashika silaha. Katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kundi la Museveni likashinda na kutwaa serikali tangu mwaka 1986.

Museveni alichaguliwa rais katika kura ya vyama vya upinzani vya 1996 na 2001.

Mwaka 2005 ulikuwa na uchaguzi wa vyama vingi vya kwanza. Museveni alipata kibali cha bunge kwa badiliko la katiba lililomruhusu kugombea urais tena mwaka 2006 akichaguliwa mara ya tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.