Pata taarifa kuu
UGANDA

Uganda yalegeza masharti dhidi ya janga la Covid-19

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kufunguliwa tena kwa maeneo ya kuabudu, lakini pia watu wanaohudhuria sherehe za harusi, idadi sasa itakuwa 200.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni. © AFP - Sumy Sadurni
Matangazo ya kibiashara

Museveni ametangaza kulegeza masharti haya katika vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.

Hata hivyo, Shule bado hazijafunguliwa nchini humo kwa kile ambacho serikali inasema, inalenga kuwapa chanjo watu Milioni 4.8 kabla ya masomo kurejelewa.

Sekta ya elimu itafunguliwa tena mnamo Januari 2022, isipokuwa vyuo vikuu na taasisi zingine za elimu ya juu, ambazo zitafunguliwa kutoka Novemba 1.

Katika hotuba ya kitaifa iliyopeperushwa kwa njia ya televisheni Jumanne, Rais Yoweri Museveni alisema kuwa kuna dozi za chanjo milioni 2.2 za Covid 19 zinazopatikana nchini kwa sasa, na wastani wa milioni kumi zaidi zinatarajiwa kuwasili katika miezi ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.