Pata taarifa kuu
UGANDA-AFYA

Wabunge wa Uganda wazuiwa kuingia bungeni kwa kipindi cha wiki mbili

Wabunge nchini Uganda, wametakiwa kutokwenda katika majehgo ya bunge kwa kipindi cha wiki mbili, kufuatia ongezo la maambukizi ya virusi vya Covid 19 wakati huu nchi hiyo ikiwa imefungwa kwa siku 42.

Majengo ya Bunge la Uganda.
Majengo ya Bunge la Uganda. CC/Andrew Regan
Matangazo ya kibiashara

Aina mpya ya virusi vimeelezwa kuwa chanzo cha ongezeko la mamabukizi hayo katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki ambayo ina maambukizi zaidi ya Elfu 40 na vifo zaidi ya 300 tangu mwaka uliopita.

Mwandishi wetu wa Kampala, Kenneth Lukwago anasema hatua hiyo inatokana na kwamba baadhi ya wabunge walipatikana na virusi vya Covid 19 licha ya kuwa idadi ya walioambukizwa haijajulikana.

Baadhi ya taarifa zinasema ni karibu wabunge 100, licha ya hivi karibuni serikali ilitangaza makataa ya watu kutotembea kwa siku 42, ambapo hakuna kutumia gari binafsi bila ya ruhusa kutoka kwa serikali, wakati gari za safari kwa umma zikiwa zimepigwa marufuku, huku gari pekee zinazoruhusiwa kuzunguka mjini na maeneo mengine ni zile zinazotumiwa na maafisa wa usalama nchini na jeshi la polisi.

Wachambuzi wa masuala ya kijamii wanasema raia wamekuwa wakilalamikia hali ngumu ya maisha kufuatia kudorora kwa uchumi wa taifa kutokana na wimbi hili la tatu la maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.  

Wabunge nchini Uganda, wametakiwa kutokwenda katika majenho ya bunge kwa kipindi cha wiki mbili, kufuatia ongezo la maambukizi ya virusi vya Covid 19 wakati huu nchi hiyo ikiwa imefungwa kwa siku 42.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.