Kikosi cha Uganda chawekwa karatini kuelekea michezo ya Olimpiki
Kikosi cha kwanza cha timu kutoka nchini, kilichokuwa kimewasili jijini Tokyo nchini Japan Jumamosi iliyopita kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki inayoanza Julai 23, wamewekwa karatini baada ya mmoja wa makocha wao kupatikana na virusi vya Corona.
Imechapishwa:
Ripoti zinasema kuwa, kocha huyo ambaye hakutajwa alipatikana na virusi hivyo, licha ya kupokea chanjo kamili ya kuzuia maambukizi hayo aina ya Astra Zeneca kabla ya kuanza safari nchini Uganda, hakuwa na maambukizi hayo.
Kikosi hicho wa watu 10 sasa kitasalia kwenye Karatini katika hoteli yao mjini Osaka mpaka Julai 3.
Miongoni mwa wachezaji walio kwenye kikosi hicho cha kwanza, ni wale wanaoshiriki kwenye mashindano ya ngumi na maafisa wa juu wa Kamati ya Olimpiki nchini Uganda.
1⃣ month to go until the Opening Ceremony of the @Olympics! 🏃♀️ 🇯🇵#Tokyo2020 | #UnitedByEmotion pic.twitter.com/wnP8iPICC5
— #Tokyo2020 (@Tokyo2020) June 23, 2021
Mashindano ya Olimpiki yaliahirishwa kutoka mwaka 2020 mpaka mwaka 2021 baada ya kuzuka kwa janga la Covid 19 na serikali ya Japan, imekuwa ikisema haitawaruhusu mashabiki wa kigeni kuja kushuhudia mashindano hayo. Mashabiki wa ndani 10,0000 ndio wanoatarajiwa kuruhusiwa uwanjani.
Maelfu ya wachezaji kutoka mataifa mbalimbali duniani watakaoshiriki kwenye michezo hiyo, wametakiwa kupata chanjo ya kuzuia maambukizi ya Corona na hawataruhusiwa kutangamana na watu jijini Tokyo.