Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI

Sudan Kusini: Dola milioni 73 pesa za umma zapitishwa mlango wa nyuma

Zaidi ya dola milioni 73 za rasilimali za umma zimetumiwa vibaya na viongozi wa Sudan Kusini tangu mwaka 2018, imebaini ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa Alhamisi wiki hii huko Geneva. Uporaji huu mkubwa wa rasilimali za serikali unatishia mchakato wa amani ambao uko hatarini katika nchi hii changa, Umoja wa Mataifa umeonya.

Mitambo ya kuzalisha mafuta ya Paloch huko Sudani Kusini 2014. Pesa nyingi zilizoibiwa zilitokana na makusanyo ya mapato ya mafuta.
Mitambo ya kuzalisha mafuta ya Paloch huko Sudani Kusini 2014. Pesa nyingi zilizoibiwa zilitokana na makusanyo ya mapato ya mafuta. REUTERS/Andreea Campeanu
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa waandishi wa ripoti hii wanasema kiwango cha ubadhirifu wa fedha za umma nchini Sudan Kusini "kinatisha. Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imeripoti kutopotea kwa dola milioni 73 tangu mwaka 2018, pamoja na karibu dola milioni 39 katika kipindi cha chini ya miezi miwili. Na bado, kiasi hiki kinaonesha tu "sehemu ya jumla ya pesa zilizoporwa", imeonya Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.

Uporaji wa mali ya umma unawanyima Wasudan Kusini huduma za kimsingi

Umoja wa Mataifa unashutumu viongozi wa Sudan Kusini kuanzisha "mfumo usio rasmi" kwa "makusudi" wa kukusanya mapato ya mafuta, kwa rasilimali kuu ya nchi hiyo. Mfumo ambao ulifanya kazi bila "uwazi wowote" au "udhibiti huru" hata kidogo.

Ripoti hiyo inahusisha wanasiasa, maafisa wa serikali, wanajeshi, lakini pia benki za kimataifa, ambazo sehemu nyingne ya pesa imepita. Kwa upabde wa Umoja wa Mataifa unasema, mabadiliko haya sio tu yanawanyima Wasudan Kusini huduma za kimsingi, katika nchi ambayo 80% ya raia wake wanaishi katika "umasikini uliokithiri".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.