Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI

Sudan yakumbwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa iliyonyesha

Watu zaidi ya 380,000 wameathiriwa na mafuriko nchini Sudan Kusini kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Jimbo la Jonglei linaendelea kukumbwa na mafuriko na kusababisha wakazi wa jimbo hilo kuyatoroka makazi yao.
Jimbo la Jonglei linaendelea kukumbwa na mafuriko na kusababisha wakazi wa jimbo hilo kuyatoroka makazi yao. AFP PHOTO / CHARLES LOMODONG
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya kibinadamu OCHA inasema, robo tatu ya watu hao waliothiriwa ni kutoka majimbo mawili ya Unity na Jonglei.

OCHA inasema, waokoaji wanaendelea na juhudi za kuwaokoa maelfu ya watu ambao wameathiriwa na mafuriko hayo, lakini changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni hali mbaya ya barabara ambazo hazipiti.

Michael Gai, ambaye amekimbilia katika mji wa Bor na Familia yake amesema, watu wengi wanaotamani kuyahama makaazi yao wameshindwa kwa sababu ya kutokuwa na barabara zinazopitika.

Mbali na makaazi ya watu kuharibiwa, mafuriko yamesomba na kusababisha maafa ya mifugo.

Mwaka uliyopita, watu wengine zaidi ya 700,000 waliathiriwa na mafuriko nchini Sudan Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.